Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WAKUU WA NCHI WA EAC WAFANYA UZINDUZI UJENZI WA BARABARA.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Arusha, viongozi na wawakilishi wa mataifa mbalimbali hawapo pichani ambao walihudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa barabara ya Arusha -Holili/Taveta -Voi km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha, tarehe 3 March,2016.

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Masharika, Kikanda na Kimataifa na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwasilisha taarifa ya Tanzania katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km234.3.
Mhe. Rais Dkt. Magufuli na Mhe.  Rais Uhuru Kenyata wakiongoza zoezi maalum la kukata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Mradi wa barabara Arusha-Holili/Taveta-Voi, wakiwa pamoja na wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na viongozi mbalimbali walioshiriki hafla fupi ya Uzinduzi huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Magufuli na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (Nairobi)  Gabriel Negata wakimwagilia maji mti mara baada ya zoezi la uzinduzi wa barabara.

Mhe. Rais akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa nchi wa wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na viongozi wawakilishi wa mataifa mbalimbali walioshiriki uzinduzi huo.

Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiagana na Mhe. Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe tayari kwa kuanza safari ya kurudi nchini Uganda mara baada ya kukamilisha shughuli zilizoambatana na Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyata akitoa neno la shukuran kwa waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhungo kuishukuru Serikali ya Tanzania tayari kwa safari ya kurudi nchini Kenya mara baada ya kukamilisha ushiriki wa Mkutano na kuzindua mradi wa ujenzi wa barabara unayoiunganisha nchi ya Kenya na Tanzania.

Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ally Mohamed Shein akiondoka katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa safari ya kuelekea visiwani Zanzibar mara baada ya kukamilisha zoezi la uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha -Holili/Taveta-Voi uliofanyika Tengeru nje kidogo ya Jiji la Arusha, tarehe 3 Machi,2016.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top