Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence
Museru (kushoto) akisoma hotuba maalum juu ya uzinduzi huo wa wadi ya
wagonjwa Mahututi (ICU). Anayefuatia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mheshimiwa Dk. Hamisi Kigwangalla
ambaye alikuwa mgeni rasmi. Wengine ni wadau waliowezesha kwa wodi hiyo
akiwemo Rais wa shirika la Gastrenterology, Prf. Meinhard Classen (wa
tatu kutoka kushoto) pamoja na Bingwa wa Magonjwa ya tumbo kutoka Misri,
Prf. Abdel Meguid.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mheshimiwa
Dk. Hamisi Kigwangalla akifafanua jambo katika mkutano huoleo wakati
alipokuwa mgeni rasmi mapema leo Machi 3.2016.
Dk.Kigwangalla akiwasili katika jengo la Mwaisela kwa ajili ya uzinduzi wa wodi ya wagonjwa Mahututi.
DK. Kigwangalla akisalimiana na mmoja wa wadau wa sekta ya afya wakati alipowasili katika jengo la Mwaisela
Dk Kigwangalla akijadili jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prf. Museru
Dk. Kigwangalla akisalimiana na mmoja wa wageni waalika katika tukio hilo
Prf.Maseru akijadiliana jambo na Rais wa shirika la Gastrenterology, Prf. Meinhard Classen (kushoto) na Dk. John wa JKCI.
Mlango huo wa kuingia ICU kabla ya uzinduzi rasmi.
Dk.
Kigwangalla akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa wadi ya wagonjwa
mahututi (ICU) katika jengo la Mwaisela. Wanaoshuhudia ni Rais wa
shirika la Gastrenterology, Prf. Meinhard Classen (kulia) na Prf. Museru
kushoto.
Dk.
Kigwangalla pamoja na viongozi wengine wakiwa ndani ya ICU baada ya
uzinduzi huo. Wengine ni Rais wa shirika la Gastrenterology, Prf.
Meinhard Classen (kushoto) na kulia ni Prf. Museru ambaye ni Kaimu
Mkurugenzi wa hospitali hiyo.
Dk.
Kigwangalla akizungumza na wanahabari muda mfupi baada ya uzinduzi huo
wa wadi ya wagonjwa mahututi katika jengo la Mwaisela. (Picha zote na
Andrew Chale.)
SERIKALI
imesema kwa sasa itakuwa ikihudumia wagonjwa wote ndani ya nchi ikiwemo
wale wagonjwa Mahututi ambao awali walikuwa wakipelekwa nje ya nchi. Hii
ni baada ya kuendelea kuimarisha huduma hizo pamoja na kuwa na wataalam
wa kutosha ambaio watapatiwa mafunzo zaidi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mheshimiwa Dk. Hamisi Kigwangalla wakati
wa kuzindua rasmi wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU) iliyopo katika jengo
la Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es
Salaam.
Dk.Kigwangalla katika uzinduzi huo, amewapongeza watendaji wote
waliofanikisha ikiwemo uongozi uliopita na ule wa sasa, Serikali pamoja
na wadau wa sekta hiyo ya afya walioguswa na kuchangia upanuzi wa huduma
za tiba ya wagonjwa hao Mahututi ambayo imewezeshwa kuwa na vifaa tiba
vya kisasa huku ikiongezwa vitanda kutoka 8 hadi 25 kwa sasa.
Aidha, Dk. Kigwangalla ametoa shukrani ya kipekee kwa wadau
waliojitolea kwa moyo wao kuchangia huduma hiyo ya wagonjwa Mahututi
ikiwemo Shirika lisilo la Kiserikali la Gastrenterology Foundation
kutoka Ujerumani na wadau wote kwa kuweza kufanikisha huduma hiyo kuweza
kupatikana hapa nchini na kupunguza safari za nje ambazo zimekuwa
zikiigharimu Nchi fedha nyingi.
Post a Comment