TIKITImaji ni miongoni mwa matunda yanayopatikana kwa wingi nchini ni
tunda lenye virutubisho vingi vyenye faida kubwa katika mwili wa
binadamu japokuwa asilimia 92 ya tikitimaji huwa ni maji.
Hata hivyo, asilimia 8 zilizobaki zina faida kubwa mwilini jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi. Tutaeleza baadhi ya faida chache kati ya tikitimaji.
Ndani ya tunda hili kuna Vitamin A, inayosaidia kuboresha afya ya
macho na pia kuondosha sumu mwilini; Vitamin C, inasaidia kuboresha
kinga, kuponya majeraha, kukinga uharibifu wa seli, kuboresha afya ya
meno na fizi; na vitamini B6, inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia
kuibadilisha Protini kuwa nishati.
Tunda la tikitimaji lina kiwango kikubwa cha Lycopene kuliko tunda lolote au mboga za majani.
Ndani ya tunda hili kuna madini ya Potasium. Lina uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.
Tikitimama pia lina Amino Asidi na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko wa damu kwenye mishipa yake.
Sifa ya kipekee iliyopo katika tunda hili ni ule uwezo wake wa
kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kwa
kunywa juisi yake iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda yake,
kutaisadia kabisa kuondoa tatizo hilo.
Tunda hili limeonesha kulainisha vizuri mishipa ya damu na kufanya
mzunguko wa damu mwilini kuwa mwepesi bila athari yoyote mbaya.
Kwenye tikitimaji kuna faida tangu kwenye majani, ganda na tunda na hata nyama yake.
Potassium iliyomo kwenye tikitimaji, huimarisha misuli ya mwili na huwafaa sana wanamichezo. Ulaji wa kipande kimoja baada ya kufanya mazoezi, huondoa tatizo la kukaza kwa misuli ya miguu, pia husaidia kupunguza uzito mwilini.
Tikitimaji lina kiwango kidogo sana cha kalori lakini lina kiwango
kikubwa cha maji, hivyo kwa mtu anayetaka kupunguza uzito wa mwili
linaweza kumsaidia kwa kula kwa wingi ambapo atakuwa anajisikia tumbo
kujaa lakini bila kuwa ameshiba sana, hivyo kuwa rahisi kwake kujizuia
na kula vyakula vingine hata kwa kutwa nzima na bila kuathirika kiafya.
Kirutubisho cha ‘Arginine’ kilichomo kwenye tikitimaji huchochea kwa
kiasi kikubwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Huondoa sumu mwilini,
vilevile hufanya kazi muhimu ya uponyaji vidonda na kuondoa ‘Ammonia’ na
sumu nyingine mwilini ambazo zinapozidi humfanya mtu kusikia uchovu na
kusababisha ugonjwa wa ini na figo.
Tikitimaji pia hufaa kuliwa na wagonjwa wa presha kwani hushusha
shinikizo la juu la damu, huongeza nuru ya macho, hutoa kinga kubwa
dhidi ya magonjwa nyemelezi yakiwemo yale hatari kama vile kansa ya
matiti, kibofu cha mkojo, mapafu na kansa ya tumbo.
Post a Comment