Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MANENO YA LE MUTUZ BAADA YA LE SUPER MAMA KUONDOLEWA WADHIFA WA UKUU WA MKOA SHINYANGA


Jina lake la kuzaliwa ni William Malecela na jina lake maarufu la mitandaoni ni Le Mutuz ambaye ni mmiliki wa williammalecela.com na jana April 11 2016 aliamua kuwajibu wanaomuandama kutokana na uteuzi wa ukuu wa mkoa wa Shinyanga chini ya Anne Kilango Malecela ambaye ni mama yake  kutenguliwa.


Le Mutuz Aliandika: "Guys naomba kusema hivi nimepigania Rais Magufuli kuwa Rais na ninamuunga mkono kwa juhudi zake za kusafisha uozo hata kama unamuhusu Mama yangu mzazi kwa sababu hata mimi wafanyakazi wa Kampuni yangu wasipofuata masharti yangu kama muajiri ni lazima niwaondoe sasa Nina wafanyakazi 4 ambao ili kuwa nao nilipitia kama watu 100


"Now nimesikia kwamba Mama yangu hakufuata masharti ya muajiri wake so amefukuzwa kazi kwangu sina pingamizi wala ishu na Rais kwa sababu Sheria ni msumeno inatakiwa kukata kote….now naona maneno mengi sana ambayo hayana UKWELI wala Msingi ndani yake


"Nimekaa Majuu Miaka 30 nimerudi Bongo nimesota nimeanzisha Kampuni yangu ya BLOGU YA WANANCHI MEDIA COMPANY LTD na sasa hivi nipo njiani kuhamia kwenye RADIO na TV now katika Maisha yangu sijawahi kuishi kwa kumtegemea mtu ila ninaishi kwa kumtegemea MUNGU‘


"Nilikuwa nafagia Majuu na pia nahangaika Baharini wakati Baba yangu Makamu wa Rais na Waziri Mkuu Leo eti Maisha yangu yataharibika kwa sababu Mama yangu sio RC? hahahaha imenichekesha sana hizi CHUKI guys zitawaua bure mnazitoa wapi? ….I mean Jana nimerudi Nairobi na sasa najitayarisha kwenda South Africa weekend hii na nikirudi ni safari ya Dubai eti Mama yangu kuwa RC wa Wiki Mbili Shinyanga kunahusika na Maisha yangu hapa Mjini Downtown na hizi Safari zangu za kikazi?


"Hahahahahaha imenichekesha sana guys nimeshasema Mara nyingi kwamba ninajua sana kwamba uhusiano wa Public na Watu Maarufu huwa ni feki ila sikutegemea kwamba watu wanaweza kuwa na CHUKI za mpaka kulazimisha kwamba eti u RC wa Mama yangu kwa Wiki Mbili tu unahusika na Maisha yangu hapa Downtown kwamba Nina Ofisi


"Apartment na Kampuni kwa sababu Mama yangu alikuwa RC wa Shinyanga kwa Wiki Mbili tu na sasa Maisha yangu yataisha HAHAHAHAHAH jamani this is the best joke of my life….otherwise guys nimewasikieni ila ninasimama na Rais Magufuli na I feel sorry for my Mum ila ni Kawaida in life na Sheria ni msumeno ….otherwise Lov U guys HAHAHAHAHa and I am Super Humbled U know" – le Mutuz Nation
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top