Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Warioba |
Aidha Warioba amewataka viongozi wa vyama vya upinzani kuhakikisha yale wanayotaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iwafanyie, wao pia wayafanye kwenye vyama vyao.
Warioba, amesema nchi inatakiwa kuangalia na kujadili kwa kina ili uchaguzi usiwe bidhaa inayotafutwa kwa fedha kama ambavyo ilijitokeza katika uchaguzi wa mwaka jana ambao alisema rushwa ilitumika kwa kiwango kikubwa.
Akizungumza katika mdahalo wa kitaifa kuhusu uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana, Warioba pia amezitaka asasi za kiraia kuwa makini na wafadhili wao kuepuka kuingiza matakwa yao binafsi kwenye siasa za ndani.
Katiba mdahalo huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam, kwa kuandaliwa na Mpango wa Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, (LHRC), Warioba amepongeza utendaji wa Rais John Magufuli, akisisitiza kuwa, uchaguzi mkuu ulikuwa na hamasa ambayo haijapata kutokea lakini ulikuwa huru na ulimalizika kwa amani na utulivu .
Post a Comment