Taarifa za hivi karibuni kutoka katika serikali ya China kuwa Tanzania
itapewa kiasi kikubwa cha fedha cha dola bilioni 20 ambazo China
imezitenga kwa ajili ya kuzisaidia nchi za Afrika kufanya mapinduzi ya
kiuchumi, inaonyesha ushirikiano mkubwa uliopo kati ya nchi hizi mbili.
Benki ya Dunia imeonya kuwa, kuongezeka kwa ushirikiano wa kiuchumi
baina ya Tanzania na China kunaweza kuathiriwa na kushindwa kukua kwa
Beijing.
China ni moja kati ya wabia wakubwa wa biashara na Tanzania na hutoa
fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo na pia imewekeza nchini. Mwaka
2014 inakaririwa kuwa thamani biashara ya Sino-Tanzania iliongezeka
thamani hadi kufikia dola bilioni 2.6 kutoka kiwango kidogo
kilichokuwepo mwaka 2000.
Katibu Mkuu katika Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Adelhelm
Meru, alisema Tanzania inatumia nafasi ya mapinduzi ya viwanda China kwa
kuhakikisha uwekezaji unafanyika kwenye vitu vitakavyoisaidia nchi.
Aidha aliendelea kueleza kuwa ifikapo mwaka 2020 sekta ya viwanda itakuwa inachangia asilimia 15 ya pato la taifa.
Katika ripoti ya uchumi nchini Tanzania yenye jina, The Road Less
Travelled: Unleashing Public-Private Partnerships in Tanzania, Benki ya
Dunia ilibaini kuwa kwa miaka ya hivi karibuni uchumi wa China umekuwa
ukikua kwa kasi ndogo. Hili ni onyo kwa Tanzania ambayo ushirika wake na
Beijing umekuwa ukizidi kila iitwapo leo.
Fedha za China katika miradi ya maendeleo ya Tanzania zimezidi
kuongozeka kila baada ya mwaka ikiwa ni pamoja na dola bilioni 1.2,
2013/14-2014/15 kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi toka Mtwara hadi
Dar es Salaam. Ripoti ya iwekezaji wa China nchini Tanzania imeongezeka
maradufu, unakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 60 kwa mwaka 2013
Kuyumba kwa uchumi wa China kuna weka katika mashaka uchumi wa Tanzania
ambapo unategemea sana uwekezaji toka China. Benki ya Dunia ilieleza
kuwa kuyumba kidogo kwa uchumi wa China kunaweza kutaiathiri tanzania
moja kwa moja au vingine kupitia uwekezaji.
China imechaangia asilimia 10 ya bidhaa zote zinazotolewa nje ya nchi na
ni nchi ya tatu kwa kuchukua bidhaa baada ya India na Afrika Kusini.
Chabzo: Swahili times
Loading...
Chediel . Powered by Blogger.
Post a Comment