Muonekano
wa nje ya Jengo la PPF lililopo Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya
Kimataifa vya Mwalimu Nyerere jijini Dar esSalaam (Sabasaba).
Maandalizi.
Afisa
Mafao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Tulla Mwigune (kulia) Afisa Michango
wa Mfuko huo, Saluna Aziz Ally (katikati) na Afisa Michango Glory
Maboya, wakijiandaa kuhudumia wateja leo asubuhi katika Maonesho ya
Biashara ya Kimataifa Sabasaba.
Afisa
Utafiti Neema Mjema (nyuma) na Mwanasheria wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,
Nyambilila Ndoboka, pia wakijiandaa kuweka mambo sawa kabla ya kuanza
kupokea wateja katika Bandao lao la Maonesho kwenye Viwanja vya Sabasaba
leo.
Afisa
Uwekezaji wa Mfuko huo, Jonas Mbwambo akiweka mambo sawa kabla ya
kuanza kupokea wateja katika Banda lao namba 86 viwanja vya Saba saba.
Afisa
Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Pauline Msanga, akitoa maelezo
kwa wananchi kuhusu Huduma za uendeshaji Mfuko huo, wakati
walipotembelea katika Banda lao lililopo kwenye Viwanja vya Sabasaba
jijini Dar es Salaam, leo.
Sehemu
ya wananchi waliotembelea Banda la Mfuko wa Pensheni wa PPF wakipata
elimu kuhusu Mafao yatolewayo na Mfuko huo na jinsi mwanachama
anavyoweza kujiunga na kuchangia.
Afisa Michango wa Mfuko huo, Saluna Aziz Ally, akimfafanulia mwanachama wake kuhusu uchangiaji wa michango ya Wanachama,
Afisa
Huduma kwa Wateja wa PPF, Mwajuma Msina, akizungumza na Mwananchi
aliyefika kutembelea Banda hilo wakati akimwelezea kuhusu huduma
zinazotolewa na Mfuko huo.
Afisa Mafao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Tulla Mwigune (kulia) akifafanua jambo kwa mstaafu wa PPF.
Mtaalamu
wa Mifumo ya Habari wa Mfuko wa PPF, Isabela Ngalawa, akimwelekeza
mmoja kati ya Wanachama wa Mfuko huo kuhusu 'PPF Taarifa Mobile Apps'
ili mwanachama aweze kupata taarifa za michango yake kupitia simu yake
ya mkononi.
Afisa
Huduma kwa Wateja, Mohamed Siaga, akizungumza na Mwananchi aliyefika
katika Banda la PPF kuhusu jinsi ya kujiunga na Mfumo wa 'Wote scheme
kutoka sekta isiyo rasmi.
Mmoja
kati ya Wanasheria wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Nyambilila Ndoboka,
akimwelekeza jambo mwanachama wa Mfuko huo kuhusu masuala ya Kisheria,
wakati alipofika kutembelea Banda la Maonesho la PFF leo.
Afisa
Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Temeke, Sostenes Lyimo
(kushoto) akifafanua jambo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea Banda
hilo.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiwa katika picha ya
pamoja mbele ya Banda lao Namba 86 lililopo katika Viwanja vya Sabasaba.
Picha Zote na Mafoto Blog
Picha Zote na Mafoto Blog
Post a Comment