RAIS Dk. John Magufuli, ametengua uteuzi wa ma-DC watatu wateule wa Wilaya za Rombo, Serengeti na Ikungi.
Kwa upande wa Wilaya ya Ikungi, alisema wakati wa kuandika majina ilikosewa badala ya Miraji Mtaturu ikaandikwa Fikiri Said.
Pia ametengua uteuzi wa Fatma Toufiq aliyepangiwa Wilaya ya Rombo na nafasi hiyo kupewa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Agness Hokororo.
“Makosa yaliyofanyika Rombo, tulimteua Fatma Toufiq ambaye alikuwa DC wa Manyoni lakini kumbe ni mbunge tayari, kwa hiyo tumempeleka mama Hokororo hii ni kwa sababu sikutaka mtu awe mbunge halafu awe DC… kazi moja, mtu mmoja ili pawe na effectiveness (ufanisi) kwenye kazi na ndiyo maana ya Hapa Kazi Tu,”alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli pia alitengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Emile Ntakamulenga na badala yake nafasi hiyo imechukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu.
AAIBIKA
Katika hatua nyingine wakati wakuu hao wa wilaya wakila kiapo cha maadili mbele ya Kamishna wa Maadili ya Utumishi wa Umma, Jaji Salome Kaganda, Ntakamulenga ambaye alihudhuria hafla hiyo akijua kuwa na yeye ni DC, alitakiwa kutoka nje na kuwapisha waliokuwa wakiapishwa kwa kuwa aliteuliwa kimakosa.
CHANZO:Mtanzania
Post a Comment