Msanii mkongwe wa muziki, Abbas Hamisi Kinzasa ‘20%’ amerudi katika
label yake ya zamani ‘Combination Sound’ inayosimamiwa na mtayarishaji
mkongwe wa muziki nchini Man Water.
20% akisaini mkataba mbele ya Man Water pamoja na mwanasheria
Muimbaji huyo ambaye mwaka 2011 alitwaa tuzo saba za Kilimanjaro
Music Award (KTMA) kwa mara moja, huku producer wake Man Water akichukua
tuzo mara mbili mfululizo za producer bora (mwaka 2013 na 2014), tayari
amesharekodi ngoma kadhaa chini ya producer huyo.
Kupitia instagram, Man Water ameandika: Twenty Percent is back 2016,
kaa mkao wa kula ngoma zenye jumbe nzito na za kusisimua, kila kitu kiko
sawa sasa, new page.
20% kwa sasa anajipanga kuachia wimbo wake mpya utaotoka Julai 18
mwaka huu huku akijapanga kuandaa albamu yake iitwayo ‘Sauti ya
Gharama’.
Post a Comment