Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

BILIONEA MO DEWJI AWASILISHA RASMI BARUA YA KUINUNUA KLABU YA SIMBA



BILIONEA  Mohamed Gulam Dewji amesema kuwa amewasilisha leo barua rasmi ya kutaka kununua hisa 51% klabu ya Simba ya Dar es Salaam.Hatua hiyo amechukua baada ya wanachama wa Klabu ya Simba kuonyesha shauku ya kutaka mnazi huyo wa Simba kuwekeza klabuni hapo.Mkutano Mkuu wa mwaka wa Simba SC jana kuridhia mabadiliko kwa kuingia kwenye mfumo wa kuuza hisa.

Mo Dewji ambaye shauku yake kubwa ni kuona Klabu ya Simba ikipata mafanikio Makubwa katika Ligi pia na Barani Afrika.Pia kuondokana na unyonge kutoka kwa mtani wao wa Jadi Yanga mabo wamekuwa na mafanikio kwa kipindi kirefu sasa ndani na nje ya uwanja.

Mo Dewji, tajiri namba moja kijana Afrika kwa mujibu wa jarida la Forbes la Marekani, ameyasema hayo asubuhi ya leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari, jengo la Godlen jubilee Towers, Mtaa wa Ohio, Dar es Salaam. 



“Leo asubuhi kitu cha kwanza nimefanya ni kuandika barua na kuipeleka ofisini kwa Rais wa Simba, Evans Aveva. Na nimefika nimekuta ofisi yake haijafunguliwa, ikifunguliwa ataikuta barua ya kwanza ni yangu pale,”amesema Mo Dewji.


Mo amesema katika barua hityo ameandika kwamba yeye ni mwanachama aliyewahi kuwa mfadhili wa timu, ambaye sasa anataka awekeze Sh. Bilioni 20 kwa kununua asilimia 51 ya hisa za klabu.

“Nimesema fedha hizo zitawekwa kwenye akaunti maalum na hazitaguswa. Nataka mchakato huu utimie ndani ya miezi mitatu kama inawezekana,”amesema. 

Hata hivyo, Mo amesema anasikitika baadhi ya viongozi wa Simba chini ya rais Aveva wanaonekana hawataki mabadiliko.

“Jana nilikuwa nafuatilia mkutano, nilisikia hoja kadhaa kwa namna moja au nyingine, ziliniumiza na zilikuwa za upotoshaji. Wanasema natangaza kwenye vyombo vya habari tu, hatujawahi kukutana. Leo niwe muwazi zaidi, nimekwishakutana na Aveva zaidi ya mara tatu. Na amewahi kuja ofsni kwangu zaidi ya mara tatu. Alikuja na (Geoffrey Nyange) Kaburu (Makamu wa Rais).  

Hizi dhana tunamsikia Mo kwenye vyombo vya habari si za kweli,”. 

“Lakini pia, kulikuwa kuna hoja Mo anasema kwa maneno si kwa maandishi, sisi tulikuwa tunangojea wanachama waridhie mabadiliko ya mfumo, kwa kuwa wameridhia na ninawashukuru sana. 

Leo asubuhi kitu cha kwanza nimefanya ni kuandika barua na kuipeleka ofisini kwa Rais wa Simba, Evans Aveva,”amesema na kuongeza. “Sasa barua kapata, nitamuomba Evans ajaribu kukaa na Kamati ya Utendaji, ili waone namna ya kufanikisha hili jambo haraka,”aliongeza Dewji.

Aidha, Dewji alisema ahadi yake ya kusaidia usajili wa wachezaji Simba SC wakikubali mabadiliko iko pale pale. “Ahadi yangu iko pale pale, lakini lazima viongozi waridhie,”alisema.

Katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Simba SC uliofanyika jana, uongozi uliridhia ombi la wanachama kutaka mabadiliko na kuingia kwenye mchakato huo mara moja.

Na wanachama walishinikzia mabadiliko baada ya Mo Dewji kutangaza ofa ya kununua asilimia 51 ya hisa za klabu kwa Sh. Bilioni 20 na kuwekeza.

Na Mo ameahidi kuifanya Simba iwe klabu bora zaidi nchini iwapo atafanikiwa kupewa hisa pia kuwawezesha mashabiki wa klabu hiyo kumiliki shea.

Wazo hizo la Mo dewji linakutana pia na vizingiti lukuki kutoka kwa wadau mbalimbali wengi wakihoji kwanini asianzishe timu yake? Jambo ambalo amelisemea na kusema amevutiwa zaidi na idadi kubwa ya mashabiki wa timu ya Simba.

Pia friends of Simba nao wanaonekana hataki mpango huu wa Mo dewji mpango unaonekana utawazuia wao kuwa na sauti ndani ya Klabu hiyo na kundi la wazee wa Kalbu ya Simba likipinga kabisa hiyo yote ni kile kinachoonekana ni suala la maslahi kwa pande zote  mbili.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top