Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

PICHA:SIMBA ILIVYOJIFUA KUJIANDAA NA NUSU FAINALI DHIDI YA AZAM FC

Kikosi cha Simba kimehamia mji wa Unguja ambako mchezowa nusu fainali kombe la mapinduzi dhidi ya AzamFC utapigwa. Simba imepeleka wachezaji wake wote muhimu 
kuelekea mchezo wake na Azam utakaopigwa hapo kesho saa 2:15 usiku kwenye dimba la Amaan. Hizi ni baadhi ya picha za wachezaji wakiendelea na mazoezi makali kuelekea mchezo huo.

TAARIFA KUTOKA SIMBA:OKWI FITI KUCHEZA DHIDI YA STAND UNITED


 

Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Emmanuel Okwi, anatarajiwa kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United utakaopigwa tarehe 4 Machi,siku ya Ijumaa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Simba katika kurasa za mitandao ya kijamii jana Jumanne, Daktari wa timu, Yassin Gembe, pamaja na Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema, Okwi anaendelea vizuri na huenda akacheza kwenye mechi yao ya Ijumaa dhidi ya Stand United endapo kocha ataamua kumtumia wamesema hali ya mchezaji huyo inaendelea vizuri na kuna asilimia kubwa ya kucheza Ijumaa.

''Okwi anaendelea vizuri sana tofauti na jana, kwa hali aliyonayo pamoja na tiba ambazo tumeshampatia ni asilimia kubwa sana kwa yeye kuwepo kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Stand United Ijumaa hii'' alisema Gembe.

Huku afisa habari naye akiandika kwenye kurasa yake kuwa “Okwi anaendelea vizuri aligongwa kidogo kwenye enka lakini anaendelea vizuri, kama mambo yatakuwa vizuri kesho atakuwa mazoezini. Wanachama wa Simba na mashabiki wasiwe na hofu, alipata jeraha dogo ambalo haliwezi kumsababishia akose mchezo unaokuja kama kocha ataamua kumtumia”-Haji Manara, afisa habari Simba.

Okwi aliumia katika mchezo uliopita dhidi ya Mbao FC katika ligi, na kupelekea kutolewa nje huku nafasi yake ikichukuliwa na Laudit Mavugo.

Mpaka sasa Okwi amefunga jumla ya mabao 16 katika michezo 19 ambazo Simba imecheza mpaka sasa katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

“Timu inaingia kambini kesho kujiandaa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Stand United Ijumaa Machi 2, 2018.”


SIMBA YAISHUSHIA KIPIGO MBAO,OKWI AKIZIDI KUWIKA

Simba imezidi kujikita kileleni mwa VPL baada ya kuishushia kipigo cha mbwa mwizi timu ya Mbao Fc kwa mabao 5-0 katika Uwanja wa Taifa.Ubabe wa Simba michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuipa dozi nene.

Katika mchezo huo ambao Simba waliutawala kwa asilimia kubwa, walianza kutikisa nyavu zake katika dakika ya 37 kupitia Shiza Kichuya, na dakika chache baadaye Emmanuel Okwi alifunga bao la pili kwa njia ya penati, baada ya kuchezewa faulo ikiwa ni dakika ya 41.

Mpaka dakika 45 za awali zinamalizika, Simba walikuwa kifua mbele kwa mabao 2-0.Huku ikionekana dhahiri shahiri Mbao Fc haikuwa siku yao hiyo.Simba ingevuna mabao zaidi iwapo umakini ungezingatiwa zaidi.

Kipindi cha pili kilianza  Simba wakionesha uchu wa kufunga zaidi, ambapo 69, Emmanuel Okwi alifunga tena bao, na kufikisha mabao mawili kwenye mchezo huo.

Na katika dakika ya 82, Erasto Nyoni aliongeza bao la 3, na baadaye kuelekea mwishoni mwa mchezaji, Nicoulous Gyan akapigilia msumari wa mwisho, kwa kufunga bao la 5.

Mpaka dakika 90 zinamaliza, Simba SC 5-0 Mbao FC.


Katika mchezo huo mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi ameivunja rekodi ya Simon Msuva na Abdulrahman Musa baada ya kufikisha magoli 16 kwenye ligi kuu Tanzania bara ikiwa ni mzunguko wa 19 raundi ya pili msimu huu (2017/18).

Ikizingatiwa mfungaji wa msimu uliopita 2016/17 waliangoza kwa mabao 14.

BAADA YA KUSONGA MBELE MICHUANO YA AFRIKA SIMBA KUTUA KIBABE LEO


Baada ya ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Gendarmerie, Wekundu wa Msimbazi wanatajiwa kutua nchini kibabe.

Simba SC ilikuwa nchini humo kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika CAF dhidi ya Gendarmerie na kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 1 – 0 bao likifungwa na mshambuliaji wao raia wa Uganda, Emmanuel Okwi katika kipindi cha pili.

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo umeseme kuwa Simba itaondoka Djibouti majira ya saa 12:05 jioni.
Kikosi cha Simba kurejea leo nchini.
Kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka nchini Djibouti saa 12:05 jioni ya leo kurejea nchini kwa kutumia usafiri wa ndege kupitia Shirika la KQ.
Simba SC imefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo mikubwa Afrika kwa ngazi ya klabu baada ya kuifungashia Gendarmerie kwa jumla ya mabao 5 – 0,na sasa itakwaana na Klabu ya Misri.

MANARA:TUSIWAZOMEE YANGA TAFADHALI


Simba ni ikiwa imechimbia Kileleni mwa Vodacom Premium League Uongozi wake umetoa rai kwa mashabiki wa  klabu hiyo kutowazomea wachezaji wa Yanga watakapokuwa wanaiwakilisha Tanzania kwenye mechi ya kombe la vilabu bingwa Afrika Jumamosi dhidi ya St. Louis Suns United kwenye uwanja wa taifa.
Hilo limesemwa na Afisa habari wa Simba Haji Manara, ''hawana undugu na Yanga lakini mashabiki wa Simba wasiwazomee kwa sababu watakuwa wanawakilisha nchi''.
“Nawaomba mashabiki wa Simba wasiende kuizomea Yanga kwenye mechi yao ya kimataifa siku ya Jumamosi, kama hawawezi wasiende uwanjani. Sisi sote ni wawakilishi wa nchi, tunapofungwa na timu kutoka nje hawasemi wameifunga Yanga au Simba wanasema wameifunga Tanzania”-Haji Manara.
“Yanga si maadui zetu, ni watani zetu, ‘kucharurana’ kubaki kwenye mechi zetu za hapa nyumbani, kama wao watatuzomea ni wao siwezi kuwaomba wasifanye hivyo.”
Msemaji huyo mwenye maneno mengi amesema Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassani Mwinyi atakuwa mgeni rasmi kwenye mechi yao ya Caf Confederation Cup dhidi ya Gendarmerie Nationale siku ya Jumapili kwenye uwanja wa taifa.
Klabu hiyo ya Simba imetangaza viingilio kwa ajili ya mchezo huo ambapo kiingilio cha chini kabisa kitakuwa ni Tsh. 5000 kwa viti vya mzunguko.Hii ni katika kuwavutia mashabiki wengi kuingia ili kuipa hamasa timu ikicheza.
Katika majukwaa mengine Viingilio vitakuwa  ni VIP A Tsh. 30,000, VIP B Tsh. 20,000, viti vya Orange Tsh. 10,000.
Simba ambayo imekosekana katika Soka la Kimataifa kwa muda mrefu inauchukulia kwa umakini sana mchezo huo.

RUVU SHOOTING YAIANGUKIA SIMBA NA KUOMBA RADHI


*Yamuomba radhi Okwi 
Uongozi wa klabu ya Ruvu Shooting inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara umeomba radhi kufuatia tukio lisilo la kiungwana la mchezaji wake Mau Bofu kumpiga kiwiko mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi.
Bofu alifanya tukio hilo katika dakika ya 43 ya mchezo uliozikutanisha timu hizo Jumapili iliyopita katika Uwanja wa Uhuru na kurushwa mbashara kupitia Azam Sports 2, na kusababisha Okwi asiweze kuendelea na mchezo na yeye kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.
Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema wao kama uongozi pamoja na mchezaji mwenyewe wamekiri kufanya kosa hilo na wanamuomba radhi Okwi mwenyewe, uongozi wa Simba pamoja na wapenda soka wote.
Kwa mujibu wa msemaji huyo, uongozi wa Ruvu Shooting umefanya jitihada za kutafuta namba ya simu ya Okwi ili kuzungumza naye moja kwa moja lakini namba waliyopewa imekuwa haipatikani.
Bwire amekiri kuwa kitendo kile kiliigharimu timu lakini mchezaji mwenyewe ameomba msamaha na kusema hakudhamiria kufanya kitendo kile bali aliteleza kulingana na mazingira ya mchezo, jambo ambalo analijutia na kuahidi kutolifanya tena.

BILIONEA MO DEWJI AWASILISHA RASMI BARUA YA KUINUNUA KLABU YA SIMBA



BILIONEA  Mohamed Gulam Dewji amesema kuwa amewasilisha leo barua rasmi ya kutaka kununua hisa 51% klabu ya Simba ya Dar es Salaam.Hatua hiyo amechukua baada ya wanachama wa Klabu ya Simba kuonyesha shauku ya kutaka mnazi huyo wa Simba kuwekeza klabuni hapo.Mkutano Mkuu wa mwaka wa Simba SC jana kuridhia mabadiliko kwa kuingia kwenye mfumo wa kuuza hisa.

Mo Dewji ambaye shauku yake kubwa ni kuona Klabu ya Simba ikipata mafanikio Makubwa katika Ligi pia na Barani Afrika.Pia kuondokana na unyonge kutoka kwa mtani wao wa Jadi Yanga mabo wamekuwa na mafanikio kwa kipindi kirefu sasa ndani na nje ya uwanja.

Mo Dewji, tajiri namba moja kijana Afrika kwa mujibu wa jarida la Forbes la Marekani, ameyasema hayo asubuhi ya leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari, jengo la Godlen jubilee Towers, Mtaa wa Ohio, Dar es Salaam. 



“Leo asubuhi kitu cha kwanza nimefanya ni kuandika barua na kuipeleka ofisini kwa Rais wa Simba, Evans Aveva. Na nimefika nimekuta ofisi yake haijafunguliwa, ikifunguliwa ataikuta barua ya kwanza ni yangu pale,”amesema Mo Dewji.


Mo amesema katika barua hityo ameandika kwamba yeye ni mwanachama aliyewahi kuwa mfadhili wa timu, ambaye sasa anataka awekeze Sh. Bilioni 20 kwa kununua asilimia 51 ya hisa za klabu.

“Nimesema fedha hizo zitawekwa kwenye akaunti maalum na hazitaguswa. Nataka mchakato huu utimie ndani ya miezi mitatu kama inawezekana,”amesema. 

Hata hivyo, Mo amesema anasikitika baadhi ya viongozi wa Simba chini ya rais Aveva wanaonekana hawataki mabadiliko.

“Jana nilikuwa nafuatilia mkutano, nilisikia hoja kadhaa kwa namna moja au nyingine, ziliniumiza na zilikuwa za upotoshaji. Wanasema natangaza kwenye vyombo vya habari tu, hatujawahi kukutana. Leo niwe muwazi zaidi, nimekwishakutana na Aveva zaidi ya mara tatu. Na amewahi kuja ofsni kwangu zaidi ya mara tatu. Alikuja na (Geoffrey Nyange) Kaburu (Makamu wa Rais).  

Hizi dhana tunamsikia Mo kwenye vyombo vya habari si za kweli,”. 

“Lakini pia, kulikuwa kuna hoja Mo anasema kwa maneno si kwa maandishi, sisi tulikuwa tunangojea wanachama waridhie mabadiliko ya mfumo, kwa kuwa wameridhia na ninawashukuru sana. 

Leo asubuhi kitu cha kwanza nimefanya ni kuandika barua na kuipeleka ofisini kwa Rais wa Simba, Evans Aveva,”amesema na kuongeza. “Sasa barua kapata, nitamuomba Evans ajaribu kukaa na Kamati ya Utendaji, ili waone namna ya kufanikisha hili jambo haraka,”aliongeza Dewji.

Aidha, Dewji alisema ahadi yake ya kusaidia usajili wa wachezaji Simba SC wakikubali mabadiliko iko pale pale. “Ahadi yangu iko pale pale, lakini lazima viongozi waridhie,”alisema.

Katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Simba SC uliofanyika jana, uongozi uliridhia ombi la wanachama kutaka mabadiliko na kuingia kwenye mchakato huo mara moja.

Na wanachama walishinikzia mabadiliko baada ya Mo Dewji kutangaza ofa ya kununua asilimia 51 ya hisa za klabu kwa Sh. Bilioni 20 na kuwekeza.

Na Mo ameahidi kuifanya Simba iwe klabu bora zaidi nchini iwapo atafanikiwa kupewa hisa pia kuwawezesha mashabiki wa klabu hiyo kumiliki shea.

Wazo hizo la Mo dewji linakutana pia na vizingiti lukuki kutoka kwa wadau mbalimbali wengi wakihoji kwanini asianzishe timu yake? Jambo ambalo amelisemea na kusema amevutiwa zaidi na idadi kubwa ya mashabiki wa timu ya Simba.

Pia friends of Simba nao wanaonekana hataki mpango huu wa Mo dewji mpango unaonekana utawazuia wao kuwa na sauti ndani ya Klabu hiyo na kundi la wazee wa Kalbu ya Simba likipinga kabisa hiyo yote ni kile kinachoonekana ni suala la maslahi kwa pande zote  mbili.

KUTOKA WEKUNDU WA MSIMBAZI PATA RATIBA YA MSIMU MZIMA 2016/17


SIUMBA WAIJIBU YANGA

Awali ya yote klabu inaendelea kutoa pongezi kwa ndugu zetu Waislaam wanaoendelea kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhani tunaamini Mwenyezi Mungu atawalipa malipo mema kwa ibada hiyo muhimu.

Ndugu wanahabari katika siku za karibuni hususan kuelekea mchezo wa Yanga na klabu kutoka Congo DRC  TP Mazembe Englebert kumekuwa na maneno mengi kutoka klabu ya Yanga yakiishutumu klabu yetu kuhusiana na kutokutoa ruhusa kwa mchezaji Hassan Ramadhani ‘Kessy’ na pia kuhusiana na namna mashabiki watakavyokaa majukwaani siku ya mchezo huo Jumanne ya wiki hii.

Klabu ya Simba kwa maksudi kabisa inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na mambo hayo mawili yanayoleta sintofahamu miongoni mwa wadau wa mchezo huu murua wa kandanda.

Hakuna barua yoyote ambayo klabu ya Yanga imetuandikia kuhusiana na suala la mchezaji Hassan Ramadhani ‘Kessy’ pia hakuna hata mazungumzo yaliyofanyika baina ya viongozi wa vilabu hivi ili kutuomba walau kwa mdomo kama taratibu zinavyotaka.
Ikumbukwe Simba huwa haina tatizo kuruhusu matakwa binafsi ya mchezaji na nyote mnajua utamaduni huo wa klabu yetu.

Kwa wasiofahamu mwaka 1998 klabu ya Simba iliwaazima wachezaji watatu Yanga ili wacheze hatua ya makundi kama hii ya klabu bingwa Afrika wachezaji hao ni Shaban Ramadhani Monja Liseki na Alphonse Modest sasa jiulize kama tuliweza kuwaazima wachezaji vipi tushindwe kumruhusu mchezaji waliyemsaini? Pamoja na maneno yao ya kuudhi Simba ni waungwana wa kutosha na wao wasitumie ukimya wetu kuwapotosha wanachama na washabiki wao eti tumewakatalia kuwajibu barua ya Hassan Ramadhani ‘Kessy’
Msimamo wetu kuhusiana na jambo hili inategemea uungwana wao tu.

Pia Yanga kupitia msemaji wao wamenukuliwa kuwa kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe watakaa kwenye majukwaa yote hata yale ambayo kwa utamaduni wa uwanja wa taifa hukaliwa na mashabiki wa klabu yetu.

Tunafahamu kuwa kauli hii ina nia ya kuchochea vurugu kubwa kwenye mchezo huo na sote tunajua athari ya vurugu michezoni tunawashauri Yanga wasijaribu kuleta mashabiki wao kwenye majukwaa wanayokaa washabiki wa Simba ili kuleta amani siku hyo ya mchezo.matarajio yetu vyombo vinavyohusika vitasimamia kwa ukaribu jambo hilo.

Mwisho ingawa si kwa umuhimu klabu haimzuii yoyote kushangilia timu yoyote siku ya mchezo huo kama zilivyo desturi ya wao Yanga kushangilia klabu yoyote inayocheza na Simba hususan wageni toka nje.kama ilivyokuwa miaka michache nyuma ambapo walishangilia na kuvaa jezi za TP Mazembe.

Waarabu wana msemo wao maarufu “KAMA TUDINI TUDANI” kama ulivyofanya na wewe utafanyiwa hivyohivyo.

Imetolewa na
Haji S Manara
Mkuu wa habari
Simba Sports Club

SIMBA MABADILIKO KUIANGUSHA PRISONS

 Simba ilikuwa imegeuka kibonde wa Kagera Sugar pamoja na timu za Tanga na Mbeya, lakini msimu huu imezigeuzia kibao.
Kocha mkuu wa Simba, Dylan Kerr.
 
 
Baada ya kuvunja mwiko wa kuwa kibonde wa Mbeya City katika misimu miwili iliyopita, benchi la ufundi la Simba limetamba litaendeleza kaulimbiu ya 'mabadiliko' inayotamba nchini kwa sasa kwa kuibuka na ushindi dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya keshokutwa.
 
 
Simba ililazimishwa sare na Mbeya City katika mechi zote mbili za msimu wa kwanza (2013/14) wa timu hiyo ya Mbeya kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), kabla ya kuchezea kichapo katika mechi zote mbili za msimu uliopita wa ligi hiyo, 2-1 nyumbani na 2-0 ugenini, lakini juzi Wanamsimbazi walianza na kikosi chenye viungo watano, Said Ndemla, Jonas Mkude, Abdi Banda, Mwinyi Kazimoto na  Justice Majabvi na kuchomoza na ushindi wa 1-0 dhidi ya timu hiyo mjini hapa.
 
 
Ushindi huo ni mwendelezo wa mabingwa hao mara 18 wa Bara kufanya mabadiliko baada ya mwanzoni mwa msimu kuvunja mwiko wa kugawa pointi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kwa misimu mitatu, safari hii wakichukua pointi sita kutoka kwa African Sports na Mgambo Shooting.
 
 
Mara tu baada ya kumalizika kwa mechi yao ya juzi jijini hapa, kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola, aliiambia Nipashe kuwa Tanzania Prisons ambao ambayo juzi ilisambaratishwa kwa kipigo kikubwa cha mabao 3-0 dhidi ya Stand United mjini Shinyanga, ijiandae kukumbwa na mabadiliko ya Msimbazi keshokutwa.
 
 
"Tumecheza vizuri kipindi cha kwanza, kipindi cha pili hali ya hewa ilitusumbua, lakini muhimu ni pointi tatu kwa sababu uwanja huu (Sokoine) umekuwa mgumu kwetu kwa kipindi kirefu. Tuko hapa Mbeya kwa ajili ya kuvunja mwiko na kupata pointi sita. Tayari tumepata tatu kwa Mbeya City, tunazisubiri pointi tatu nyingine kutoka kwa Prisons Jumatano," alitamba Matola.
 
 
Kuhusu mchezaji wa zamani wa Simba, Haruna Moshi 'Boban' ambaye juzi alicheza kwa mara ya kwanza VPL akiwa na kikosi cha City, Matola alisema: Hakuna asiyejua Boban ni mchezaji mzuri, tatizo linalomsumbua kwa sasa ni kwamba amenenepa, lakini akifanya mazoezi, atawasaidia sana Mbeya City."
 
 
Katika hatua nyingine, kocha mkuu wa Simba, Dylan Kerr, amekiponda kikosi chake kwa kuonyesha kiwango duni kwenye mechi yao ya juzi dhidi ya City.
 
 
Katika mahojiano na Nipashe jijini hapa jana, Muingereza huyo alisema: "Sijafurahishwa na namna timu ilivyocheza dhidi ya Mbeya City. Tulizidiwa kwa kiasi kikubwa, goli na ushindi pekee ndicho kitu cha kufurahia hapa, hatukucheza hivi kwenye mazoezi. Mechi haikuwa na furaha kwangu kwa sababu tumecheza soka la Amerika."
 
 
Kocha wa Mbeya City, Abdul Mingange, aliliambia gazeti hili jijini hapa juzi kuwa ili timu yake ifanye vizuri VPL msimu huu, watalazimika kusaka washambuliaji wakali wakati wa usajili wa dirisha dogo mwezi ujao.
 
 
"Tumetengeneza nafasi nyingi za mabao, lakini safu yetu ya ushambuliaji imetuangusha. Tunatakiwa kulitumia vyema dirisha dogo kuongeza washambuliaji," alisema meja huyo mstaafu ambaye msimu uliopita alikinoa kikosi cha Ndanda FC ya Masasi, Mtwara.
 
 
CHANZO: NIPASHE
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top