Baada ya Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji kutangaza kujiuzulu nafasi
hiyo, Mashabiki na wanachama wa Yanga wamekusanyika kwenye ofisi za
klabu hiyo wakipinga kujiuzulu kwa Manji.Mashabiki hao wengi wao wakieleza hawakubaliani na hatua hiyo ya Manji.
Baadhi ya wanachama na mashabiki wamekuwa wakidai kwamba kuna watu
ambao hawataki kumuunga mkono Manji katika zoezi zima la kutaka kuikodi
timu pamoja na nembo kwa miaka 10.Hivyo hao mashabiki ambao hawakubaliani na ombi la manji wametakiwa kutokwamisha mpango huo wa kumkodishia Manji timu.
Mzee Akilimali amekuwa akitajwa kuwa miongoni mwa watu wanaopinga
kusudi la mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji kuikodi klabu hiyo.Mzee Akilimali alisikika katika mahojiano na redio moja jijini Dar es salaam akipingaa mpango huo.
Post a Comment