Afisa
 wa polisi mwenye cheo cha koplo amekutwa amekufa asubuhi ya usiku 
aliyokuwa zamu katika uwanja wa Jomo Kenyatta International Airport 
(JKIA).
Kwa jina anaitwa Gaudencia Wausi (28) na
 alikutwa amejipiga risasi kichwani msalani asubuhi ya Agosti 24, wakati
 akiwa zamu katika uwanja huo wa ndege.
Ujumbe aliyouacha Afisa huyo wa polisi 
aliyejiua JKIA katika mtandao wa kijamii wa Facebook masaa matano kabla 
ya kifo chake, uliashiria kwamba marehemu alikua na mawazo ya kujiua. na
 ujumbe mwingine aliacha ulimhusu zaidi mwanaye wa kiume
“Mwanangu mpendwa, nakuombea ukue vizuri na Baraka. Nakuomba ukumbuke mie mamako nakupenda,” aliandika.
Mwili wa marehemu uligundulika na 
mfanyakazi wa usafi  wa asubuhi saa mbili asubuhi katika uwanja huo, 
siku ya Jumatano, Agosti 24, 2016.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Post a Comment