Mchezo wa hatua 16 bora kati ya Paris
Saint-German waliokuwa wenyeji wa Barcelona ni wazi umemchanganya kocha
wa Barca baada ya dakika 90 kumalizika kwa PSG kuibuka na ushindi wa
goli nne kwa bila, kipigo ambacho kinaifanya PSG kuwa timu ya sita
kuifunga Barcelona goli nne katika michezo ya Ligi ya Mabigwa Ulaya.
Luis Enrique amesema PSG walijipanga
kuwathibiti jambo lililofanya mchezo huo kuwa mgumu kwao tangu dakika ya
kwanza hali iliyosababisha kukubali kichapo cha goli nne lakini
hatakata tamaa kwani lolote linaweza kutokea katika mchezo wa marudiano.
“Ulikuwa mchezo wenye maafa
makubwa, sio ngumu kuelezea, PSG walikuwa wazuri kuliko sisi tangu
mwanzo. Walikuwa na kasi na walikuwa wazuri zaidi wakiwa na mpira. Ni
wazi tulikuwa dhaifu,
“Ninawajibika kwa hili na hakuna
mtu mwingine wa kulaumiwa. Lawama zote zinaniangukia mimi, wachezaji wao
hutupa furaha tu na bado kuna hatua nyingine siwezi kupoteza
matumaini,” alisema
Magoli ya PSG katika mchezo huo
yalifungwa na Angel Di Maria aliyefunga magoli mawili, Julian Draxler na
Edinson Cavani, mchezo wa marudiano wa Barcelona na Paris Saint-German
utapigwa Machi, 8 katika uwanja wa Camp Nou
CREDIT:MO Dewji Blog na Daily Mail
Post a Comment