Bei ya nyanya katika masoko mbalimbali Jijini Dar es Salaam imepanda kulinganishwa na hali ilivyokuwa wiki mbili zilizopita.
Kwasasa bei ya jumla imepanda kutoka shilingi elfu 35 kwa sanduku na kufikia shilingi elfu 60 tofauti na hali ilivyokuwa nyuma.
Baadhi ya madalali wamesema kuwa bei
imepanda kutokana na kiasi kidogo cha shehena ya nyanya kinachoingia
sokoni hapo kwa sasa wanategemea nyanya kutoka kwa wakulima wa Arusha,
Iringa na Makambako pekee.
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara
wadogo wanaouza nyanya kupitia vipimo vya asili maarufu kama sado,
wamesema kupanda kwa bei kumefanya biashara kuwa ngumu kwani wateja
wamekuwa hawamudu ongezeko hilo la bei.
1 comments:
Thanks for sharing, nice post! Post really provice useful information!
ReplyGiaonhan247 chuyên dịch vụ vận chuyển hàng đi mỹ cũng như dịch vụ ship hàng mỹ từ dịch vụ nhận mua hộ hàng mỹ từ trang ebay vn cùng với dịch vụ mua hàng amazon về VN uy tín, giá rẻ.
Post a Comment