Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MADRID HALI TETE BAADA YA KUNYUKWA NA ESPANYOL,KOCHA ZIDANE AZIDI KUKALIWA KOONI



Real Madrid imekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Espanyol katika Dimba la RCDE usiku wa leo katika mchezo wa La Liga.

Kipigo hicho kina maana sasa Real Madrid wameshindwa kupunguza pengo la pointi 14 dhidi ya vinara Barcelona.

Pia ni ushindi wa kwanza kwa Espanyol katika mechi 20 walizokutana na Madrid.

Mechi hiyo iliyokuwa ilichukua takribani dakika 90+ kutikiswa kwa nyavu zake, zikiwa zimeongeza dakika 3, Gerard Moreno alifunga goli ambalo limemaliza mchezo huo kwa matokeo hayo.

Madrid walikuwa dimbani bila uwepo wa Cristiano Ronaldo, sasa inakuwa katika wakati mgumu wa kuwafukuzia wapinzani wao Barcelona walio na alama 65 huku Madrid akiwa na 51.

Pamoja na hayo, Kocha Zinedine Zidane anazidi kujiwekea mazingira magumu ya kuendelea kusalia kikosini hapo msimu ujao kutokana na matokeo kutokuwa mazuri kwenye ligi msimu huu.



author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top