Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MCHEZAJI BORA WA FIFA:CRISTIANO RONALDO, LUKA MODRIC NA MO SALAH KUWANI TUZO

Cristiano Ronaldo, Luka Modric na Mohamed Salah ndio wachezaji watatu wa mwisho ambao watawania tuzo la mchezaji bora wa Fifa mwaka 2018.
Tuzo hizo zinafanyika huku mshambuliaji wa Barcelona raia wa Argentina Lionel Messi, mshindi mara tano wa tuzo la Ballon d'Or amekosa kuorodheshwa katika tatu bora.
Pia hakuna mchezaji yeyote aliyekuwa kwenye kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia.
Huku winga mreno Ronaldo ambaye ni mshindi wa mwaka 2016 na 2017, alishinda kombe la tano la ligi ya mabingwa na Real Madrid mwezi Mei kabla ya kujiunga na Juventus kwa pauni milioni 99.2.
Kiungo wa kati wa Real Madrid Luka Modric alitajwa kuwa mchezaji bora kwenye Kombe la Dunia mwaka 2018 wakati Croatia ilifika fainali dhidi ya Ufaransa.
Mo Salah anakuwa mchezaji wa kwanza wa EPL kuorodheshwa kwenye tuzo hizo kwa mara ya kwanza toka mwaka 2008, pale Cristiano Ronaldo aliposhinda. Pia ni mchezaji wa kwanza toka bara la Afrika kufika hatua hiyo ya tatu bora toka Samuel Eto'o alipojumuishwa mwaka 2005.
Mmisri Mo Salah alifunga mabao 44 huku Liverpooll ikifika fainali ya ligi ya mabingwa na kushindwa na Real Madrid.
Modric aliwashinda Ronaldo na Salah kwa kushinda tuzo la mwanamume bora wa mwaka wa Uefa wiki iliyopita.
Mshambuliaji wa England Harry Kane ambaye alishinda kiatu cha dhahabu kwenye Kombe la Dunia alikuwa kwenye orodha ya kumi bora lakini amekosa.
Didier Deschamps, ambaye aliiongoza Ufaransa, ameteuliwa kuwania tuzo la kocha wa mwaka, akiwemo raia wa Croatia Zlatko Dalic na meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane.
Tuzo hizo ni kando la Ballon d'Or, baada ya shirikisho la kandanda duniani kukata uhusiano wake na tuzo hilo mwaka 2016.
Jopo la wataalamu wa Fifa waliunda orodha ya wachezaji 10 kwa kila tuzo huku manahodha wa timu za taifa, waandishi wa habari na mashabiki wakimchagua mshindi kila kundi likiwa na asilimia 25 ya kura.
Ni wachezaji nane(8) wa EPL ambao wamewahi kushiriki tuzo za mchezaji bora wa FIFA katika historia ambao ni – Lineker, Shearer, Bergkamp, Beckham, Henry, Lampard, Ronaldo, Torres.
Wachezaji wawili 2 waafrika ambao ni – Weah and Eto'o. Weah akishinda tuzo hiyo mwaka 1995, na Ronaldo mwaka 2008.
Washindi watatangazwa tarehe 24 Septemba huko Royal Festivan mjini London
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top