Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

LIVERPOOL NI KUSUKA AMA KUNYOA


Kikosi cha Jurgen Klopp kinafanya vizuri lakini wiki hii kitaanza kupata wakati mgumu kwenye safari yao ya kuwani ubingwa tofauti na timu za Manchester United,Man City,Arsenal,Chelsea  na Tottenham Hottspur.

Baada ya michuano ya UEFA Nations League kuisha wiki hii zinaingia wiki tatu mfululizo kuelekea Oktoba kabla ya wiki ya mapumziko kwa ajili ya mechi za kirafiki za kimataifa.

Katika vinara wa EPL wanaowania ubingwa wenye ratiba ngumu ni Liverpool.Hebu tuangalia kila timu ratiba yake ilivyo .
LIVERPOOL
Ina kazi ngumu,hilo halina ubishi.Hiki ndio kipindi kinachosemwa ya kwamba ni kipimo kwa klabu hiyo kama kweli ina ubavu wa kuwani Ubingwa itakapoikabili  Tottenham Hotspur, Chelsea na Manchester City.
Ugumu umekuja pale ambapo imejikuta ina ratiba ngumu ya EPL lakini ikajikuta inaanza UEFA  na Paris Saint-Germain na kuifuata Napoli , wakati huo ikiikaribisha Chelsea katika Carabao Cup.
Lakini pia ikiwa na mechi nyumbani na Southampton, ambapo Liverpool ilishinda mara moja katika mechi nne walizokutana pale  Anfield pale timu hizo zilipokutana.
Hapo Jurgen Klopp kwa mara ya kwanza itabidi aanze kupumzisha baadhi ya wachezaji na kuanzisha wengine ili kikosi chake kiweze vuka salama katika kipindi hiki.
Hizi ndio mechi za Liverpool ambazo zinaweza kuipa picha nyingine kabisa msimu huu ambapo itaanza  Sep 15: Tottenham (A), Sep 18: PSG (H) (Champions League), Sep 22: Southampton (H), Sep 25/26: Chelsea (H) (Carabao Cup), Sep 29: Chelsea (A), Oct 3: Napoli (A) (CL),  na kumaliza Oct 7: Man City (H).

Manchester City

Wakiwa wameanza vizuri dhidi  Arsenal, inatazamiwa  City watakuwa wameshinda mechi saba dhidi ya saba watakopokuja kumenyana na Liverpool mwezi  Oktoba.
Hakuna ubishi, City ana ratiba nyepesi ya EPL, UEFA pamoja na Carabao Cup.
Mechi za City Sep 15: Fulham (H), Sep 19: Lyon (H) (CL), Sep 22: Cardiff (A), Sep 25: Oxford (A) (CC), Sep 29: Brighton (H), Oct 2: Hoffenheim (A) (CL), kabla ya kupepetana Oct 7: Liverpool (H).

Tottenham Hotspur

Tottenham wamepangiwa ratiba ngumu ya Champions League kuliko Liverpool, kwa kuangalia mechi zao mbili za mwanzo kwenye grupu lake.
Carabao Cup droo nayo imekuwa rahisi kwake dhidi ya  Lilywhites, ukichukulia mechi hiyo kupigwa pale  MK Dons.
Lakini mechi yao ya wikiendi hii dhidi ya  Liverpool, EPL itatoa nafasi kwa kocha Mauricio Pochettino kukibadilisha kikosi chake
Spur itaanza wikiendi tarehe Sep 15: Liverpool (H), Sep 18: Inter Milan (A) (CL), Sep 22: Brighton (A), Sep 26: Watford (H) (CC), Sep 29:Huddersfield (A), Oct 3: Barcelona (H) (CL), Oct 6: Cardiff (H).

Manchester United

Jose Mourinho alirekodiwa akianguka pale Wembley siku ya jumamosi imejidhihirisha vivyo hivyo kwa United ambayo imejikuta ikiangukia pua kwenye mechi za mwanzo wa msimu.
Vipigo viwili vimeifanya United ikifanya vibaya na kuzusha gumzo kubwa dhidi yake na wachezaji mahiri klabuni hapo.Hivyo kipindi hiki ndicho muafaka kuinua morali ndani na nje ya klabu hiyo.
Siku ya jumamosi inafunga safari kuifuata  Watford kibarua inachotakiwa kukimaliza vizuri ili kuiona United ikipanda nafasi zaidi  katika EPL.
Tarehe  Sep 15: Watford (A), Sep 19: Young Boys (A) (CL), Sep 22: Wolves (H), Sep 25: Derby (H) (CC), Sep 29: West Ham (A), Oct 2: Valencia (H) (CL), Oct 6: Newcastle (H).

Chelsea

Kama Liverpool, vijana wa London wameanza kwa ushindi wa  100% EPL msimu huu.
Na wana mechi mbili  dhidi ya Liverpool katika mechi zijazo ambazo ni moja ya EPL na Carabao Cup ambazo inabidi ifanye vizuri katika kampeni ya kuwa na msimu mzuri.
Swali moja linabakia ni namna gani wataweza kuhimili kucheza  alhamisi Europa Ligi na Jumapili EPL  na ni namna gani Kocha  Maurizio Sarri anayachukulia haya mashindano.
Wikiendi hii Sep 15: Cardiff (H), Sep 20: PAOK Salonika (A) (CL), Sep 23: West Ham (A), Sep 25/26: Liverpool (A) (CC), Sep 29: Liverpool (H), Oct 4: MOL Vidi (A) (EL), Oct 7: Southampton (A).

Arsenal

The Gunners  kama wanavyojulikana walianza na mechi ngumu dhidi ya City na Chelsea, lakini toka hapo wameanza kubadilika.

Mechi zao zote za EPL zitakuwa ni zile zilizo songana sana kipindi hiki.
Japokuwa, Arsenal wamepata nafuu kwenye droo ya  Europa League ukweli ukiwa watacheza London mara moja siku ya jumamosi dhdi ya  Tyneside.
Sep 15: Newcastle (A), Sep 20: Vorskla Poltava (H) (EL), Sep 23: Everton (H), Sep 26: Brentford (H) (CC), Sep 29: Watford (H), Oct 4: FC Qarabag (A) (EL), Oct 7: Fulham (A).
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top