Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Tamko Rasmi la Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo kuhusu HALI YA NCHI



Dar Es salaa, Jumanne, 06 Septemba 2016

1. Utangulizi
Jana Jumatatu, 5 Septemba 2016, Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo ilikutana katika kikao chake cha kawaida. Pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu ilipokea, kujadili na kuidhinisha Taarifa kuhusu HALI YA NCHI. Taarifa hii sasa inatolewa rasmi kwa umma. Taarifa ipo katika maeneo makubwa manne: Hali ya kisiasa, hali ya kiuchumi, umoja wa kitaifa na hitimisho.

2. Hali ya Kisiasa
Kamati Kuu imezingatia kuwa Kikatiba, nchi yetu inafuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Katiba na Sheria mbalimbali zimeanisha utaratibu wa kazi na shughuli za vyama vya siasa. Ili kuhakikisha kwamba kazi na shughuli za vyama vya siasa zinakuwa endelevu, vyama vyenye kukidhi vigezo hupewa ruzuku kupitia Bajeti ya Serikali inayopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Hata hivyo, katika awamu hii ya tano, Serikali ya Chama cha Mapinduzi imeamua kuzuia shughuli za siasa kwa kutumia nguvu ya Jeshi la Polisi na hata Jeshi la Wananchi. Kwa mujibu wa serikali ya CCM, shughuli za kiuenezi za vyama vya siasa kama vile mikutano ya hadhara, maandamano, makongamano, mijadala na hata mikutano ya ndani inapaswa kukoma mapema baada ya uchaguzi. Kisheria, huu ni uvunjifu wa Katiba na Sheria za nchi. Kisiasa, tunatambua kwamba Viongozi wa CCM wamepoteza mvuto kwa wananchi na sasa wanamsukuma Mwenyekiti wao Rais Magufuli kutumia jeshi katika kuokoa taswira ya Chama cha Mapinduzi mbele ya umma.

Kwa kuzingatia hali ya kisiasa nchini kwa sasa, Kamati Kuu ya chama chetu:
i) Tunalaani na kupinga kwa nguvu zetu zote hatua za Serikali ya Chama cha Mapinduzi za kuvunja Katiba na kujaribu kuweka pembeni utawala wa sheria.

ii) Tunapinga vitendo vinavyozidi kushamiri katika serikali hii ya CCM ya kujaribu kuendesha nchi kwa ubabe na matamko ya viongozi badala ya utawala wa sharia.

iii) Tutasimama imara, na tutaungana na vyama vingine vya siasa pamoja na taasisi zingine za kiraia katika kulinda mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, uhuru wa maoni, na utawala wa sheria katika nchi yetu

3. Hali ya Kiuchumi
Katika miaka 10-15 iliyopita, nchi yetu imejenga uchumi ambao umekuwa ukikua kwa kiwango cha asilimia 6-7 kwa mwaka katika kipindi chote hiki. Ukuaji huu wa uchumi ulitokana na juhudi za nchi katika kuvutia wawekezaji na kuchochea shughuli za uzalishaji mali kwa wananchi wenye kipata cha chini. Awamu ya tano ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi imerithi changamoto ya uchumi unaokua bila kuwafaidisha wananchi wa kawaida. Hili ndilo tulitegemea Serikali mpya ishughulike nalo.

Kamati Kuu imeshtushwa na hali ya kuanza kudorora kwa shughuli za uchumi katika kipindi cha miezi kumi ya utawala wa awamu ya tano. Kwa mfano:

a) Taarifa za Benki Kuu zilizopo kwenye tovuti yake (Quarterly Economic Review na Monthly Economic Review) kwa robo ya mwisho ya mwaka 2015 (Oktoba – Desemba 2015 ) zinaonesha kuwa kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa ilikuwa 9%. Katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 (Januari – Machi 2016) kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa ilishuka hadi kufikia 5.5%. Kiuchumi, hii inamaanisha kuwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo ya utawala wa awamu ya tano chini ya Rais Magufuli umepungua kwa 4%.

b) Shughuli za uchumi zinazohusu wananchi masikini zimeshuka kutoka kasi ya ukuaji ya 10.20% robo ya mwisho ya mwaka 2015 mpaka 2.7% katika robo ya kwanza ya mwaka 2016, ikiwa ni punguzo la 8% ndani ya kipindi kisichozidi miezi sita. Hii ina maanisha kwamba Wananchi wetu wanazidi kudumbukia kwenye ufukara kwa kasi tangu awamu ya tano ya Serikali ya Chama Mapinduzi iingie madarakani

c) Ukuaji wa sekta ya ujenzi katika robo ya mwisho ya mwaka 2015 ilikuwa 13.8% lakini ukuaji wa sekta hii katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 ilikuwa ni 4.30%, ikiwa ni tofauti ya takribani -10%. Hii ni kwa sababu uwekezaji katika sekta hii umeanza kushuka.

d) Kasi ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji imeporomoka kutoka kukua kwa 14.50% robo ya mwisho ya 2015 mpaka kukua kwa 7.9% robo ya kwanza ya 2016, ikiwa ni kuporoka kwa 7% katika kipindi cha miezi 6 tu ya kwanza ya utawala wa Rais Magufuli. Kuporomoka kwa sekta ya usafirishaji itaathiri watu wengi, wakiwemo madereva, matingo, pamoja na mama Ntilie wanaowauzia chakula. .

Kwa kuzingatia mwenendo wa hali ya uchumi katika nchi, Kamati Kuu:
a) Tunaitaka serikali izingatie sayansi ya uchumi katika kuendesha uchumi wa nchi. Uamuzi wa CCM wa kuitelekeza serikali yake kwa mwanasiasa mmoja anayedhani ndiye anayejua kila kitu na yeye kugeuka kuwa mshauri wa washauri wa uchumi itasambaratisha uwekezaji nchini na kuua kabisa juhudi za miaka 20 za kuvutia wawekezaji na kujenga uchumi shirikishi.

b) Inahimiza wananchi kuzingatia kuwa msingi wa uchumi wetu ni uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi. Msingi wa kuvutia wawekezaji ni utawala wa sheria. Juhudi za serikali ya CCM za kuua utawala wa sheria zitaua uwekezaji na kuangamiza uchumi wa nchi. Tusirihusu CCM iue uchumi wa nchi kwa maslahi yake ya kisiasa na viongozi wake.

4. Umoja wa Kitaifa
Nchi yetu imefanya juhudi kubwa katika miaka 50 iliyopita katika kujenga umoja na mshikamano wa kitaifa kwa kuhakikisha kuwa makabila, dini na baadaye vyama vya siasa tunaishi bila kukamiana. Juhudi za dhati za kupambana na ubaguzi ndiyo umekuwa msingi imara wa kujenga Umoja wa Kitaifa na amani tunayojivunia.

Hata hivyo, Kamati Kuu imezingatia kuwa utawala mpya wa Serikali ya CCM, kupitia Mwenyekiti wake mpya na Rais wa Jamhuri wa Muungo, umeanza kwa juhudi na kasi kubwa kuchokonoa na kumomonyoa misingi ya utaifa na umoja wetu. Sasa tunaye Rais asiyechagua maneno na asiyejua aongee nini na wapi. Vijana waliosoma kwa bidii katika mazingira ya shule zilizotelekezwa na serikali ya CCM anawaita VILAZA. Katikati ya uhasama mkubwa wa kisiasa na kijamii huko Zanzibar Rais wetu amefunga safari, sio kujaribu kutibu majeraha yaliyosababishwa na kuchezewa kwa sanduku la kura, bali kuchochea uhasama chini ya ulinzi wa vyombo vyetu vya dola vyenye jukumu la kulinda na kudumisha amani. Sasa Rais wetu, kupitia kauli zake, ameanza kuubomoa muungano wetu uliojengwa kwa unyenyekevu na katika mazingira magumu. Kila asimamapo kuhutubia, jambo moja la kutarajiwa kutoka katika kinywa cha Rais wetu ni matamshi yanayodhoofisha nguzo fulani ya umoja, mshikamano na undugu wetu kama taifa. Yote haya yakitokea chama chake cha CCM ama kimekaa kimya au kinachekelea. Inasikitikitisha kwamba Chama kilichoasisiwa na Mwalimu Nyerere kinamruhusu kiongozi wake kubomoa misingi ya umoja wa kitaifa na kuchochea chuki katika jamii ya watanzania.

Kwa kuzingatia mtikisiko mkubwa katika umoja na mshikamano wa kitaifa unaoendelea nchini, Kamati Kuu:
a) Tunalaani juhudi zinazofanywa na Serikali ya CCM kupitia Mwenyekiti wao za kuchochea chuki katika jamii ya watanzania na kubomoa misingi ya umoja wa kitaifa na amani ya nchi

b) Tunatoa wito kwa watanzania wote waipendayo nchi yao kusimama kidete katika kulinda misingi ya nchi yetu na kukataa chuki inayoanza kujengwa na utawala wa CCM

c) Tunatoa wito wa kipekee kwa viongozi wetu wa dini na wakuu wa nchi waliopita, hususani Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa na Mzee Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na wazee wengine wanaoheshimika katika nchi yetu wavae ujasiri wa kumuonya Mwenyekiti wa CCM kuwa juhudi zake za kuchochea chuki katika jamii yetu ya watanzania zitasambaratisha Taifa letu.

5. Hitimisho
i) Sisi kama chama cha siasa, tunaendelea kusisitiza kuwa tutaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kupambana na ufisadi na kujenga uwajibikaji nchini.

ii) Tunaamini kwa dhati kabisa kuwa kuheshimu na kulinda demokrasia na kuzingatia utawala wa sheria nidyo msingi wa mapambano dhidi ya ufisadi. Tunasisitiza kuwa mtu yeyote, wa kawaida au kiongozi, anayesema kwamba anaweza akapambana na ufisadi kwa kukanyaga misingi ya demokrasia na utawala wa sheria mtu huyo ni mwomgo na kwa kweli ni fisadi na anataka kujenga himaya mpya ya ufisadi. Mtu huyo, pamoja na mambo yake yote, yafaa akataliwe na kudharauliwa haraka!

iii) Tunasisitiza kuwa msingi wa uchumi wetu ni kuvutia uwekezaji wa ndani nan je ya nchi. Kuzingatia utawala wa sheria ndiyo msingi wa kuvutia uwekezaji. Juhuzi za hivi karibuni za serikali ya CCM za kujaribu kuua utawala wa sharia ni juhudi ovu za kuua uchumi wa nchi yetu. TUZIKATAE juhudi za kuua utawala wa sheria kwa kuwa zitaangamiza taifa letu kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb
Kiongozi wa Chama
Dar es Salaam, Jumanne 6 Septemba 2016.

ZITTO KABWE AFUNGA PINGU ZA MAISHA HUKO ZANZIBAR



Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe jana aliuacha rasmi ukapera baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake aliyemvisha pete ya uchumba miezi miwili iliyopita, ndoa na tafrija zote zilifanyika Zanzibar.

KUTOKA ACT-WAZALENDO:SASA NAWASHAURI WABUNGE MPUMZISHENI MAGUFULI



Nimetumia muda wa kutosha kumpa Ushauri wa Bure Ndugu John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) juu ya Kudumisha Utawala wa Sheria na Kulinda Demokrasia iliyopelekea yeye kuwa Kiongozi wa nchi hii. Nakumbuka Msajili wa Vyama vya Siasa alijaribu kutoa Tafsiri ya Kauli ya Rais ya Kupiga Marufuku Mikutano ya Kisiasa mpaka 2020, siku moja baada ya mimi kuandika kwenye Ukurasa huu Kushangazwa kwangu na Ukimya wa Msajili wa Vyama juu ya Kauli hiyo ya Mwenyekiti Mtarajiwa wa CCM inayopingana na Kanuni za Vyama vya Siasa za Mwaka 2007 zilizotungwa chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa. 


Hata hivyo, Kauli zilizotolewa hivi karibuni na baadhi ya Wakuu wa Mikoa juu ya Kupiga Marufuku Mikutano ya Kisiasa katika Mikoa yao zinadhihirisha wazi kwamba Msajili wa Vyama vya Siasa ndiye aliyeshindwa kumuelewa Rais Magufuli.


Ingawa Katiba ya Jamhuri ya Muungano inampa Kinga Rais kushitakiwa Mahakamani (Ibara ya 46), lakini Katiba inalipa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mamlaka ya “Kumng’oa” Rais kwenye Kiti Chake. Kwa mujibu wa Ibara ya 46A (2), Bunge linaweza kumlazimisha Rais kuachia ngazi, naye kulazimika kufanya hivyo Kupitia Azimio la Bunge, endapo atathibitika kufanya makosa yafuatayo:

(a) Ikiwa ametenda vitendo ambavyo kwa Ujumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;


(b) Ikiwa ametenda vitendo ambavyo vinakiuka Maadili yanayohusu Uandikishwaji wa Vyama vya Siasa yaliyotajwa katika Ibara ya 20(2) ya Katiba; au


(c) Ikiwa amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano…


Ukifuatilia Mwenendo tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie Madarakani, Rais amekuwa akilalamikiwa kwa Kukandamiza Demokrasia, kutumia Lugha za kudhalilisha kwa Vijana waliotimuliwa Chuo Kikuu cha Dodoma (kwa kuwaita VILAZA) na mambo mengine yanayokwenda Kinyume na Katiba ya JMT na Lengo la Kuwepo kwa Katiba hiyo kama linavyobainishwa na Ibara ya 9 ya Katiba. Tazama 9(a), 9(f) na 9(h) kwa mfano, pia rejea Hotuba ya Ndugu Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo aliyoitoa mbele ya Maelfu ya Wakaazi wa Dar es Salaam, kwenye Viwanja vya Zakhiem Mbagala 05/06/2016.


Katiba ya JMT imeeleza hatua ambazo katika Mazingira kama haya, Bunge linaweza kumfikisha Rais kwenye Kujiuzulu. Ibara ya 46A(3)(a) inaeleza kwamba Mchakato wa Kumng’oa John Pombe Magufuli (JPM) Ikulu unaweza kuanza kwa Taarifa ya Maandishi inayoungwa mkono na asilimia ishirini ya Wabunge wote Kuwasilishwa, ikieleza makosa yake. Naamini kupata asilimia ishirini ya wabunge kuanzisha huu Mchakato si suala zito, linawezekana ( Kumbuka Idadi ya Wabunge wa Upinzani).

Ingawa Mchakato huu unaweza ukapata ugumu kupitia Kamati Maalum ya Uchunguzi itakayoundwa katika mazingira haya ya Demokrasia finyu, naamini Kitendo cha Rais kulazimika kujieleza/kujitetea ni hatua muhimu sana katika Kurekebisha Nidhamu na kuwakumbusha Viongozi wa Umma kwamba HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA.

Kwa mujibu wa Ibara ya 46A (9):
“ Baada ya Taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuwasilishwa kwa mujibu wa Ibara ndogo ya 8 ( yaani 46A (8)), Bunge litaijadili taarifa hiyo na litampa fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura za Wabunge wasiopungua theluthi mbili za Wabunge wote, Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashitaka dhidi ya Rais yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika Kiti cha Rais, au kuwa mashitaka hayo hayakuthibitika”.


Nitumie fursa hii kuwaondoa hofu wabunge wa Upinzani, wasihofie idadi kubwa ya wabunge wa CCM.

Wapo wabunge wanaochukizwa na baadhi ya makosa haya kwani Ubabe huu ukiachiwa hata atakapokuwa Mwenyekiti wa Chama chao, atakandamiza Demokrasia ndani ya CCM.

Kusambaratika kwa Ukomunist zama za Vita Baridi kuliwakutanisha Mahasimu Marekani na Osama Bin Laden katika dhamira moja, japo kwa Sababu na Malengo tofauti. 

Si ajabu theluthi mbili ya Kura ikapatikana ili kulinda Maslahi mapana ya Taifa hili. 

Hivyo naamini JPM atalazimika kujiuzulu ndani ya Siku 3 tangu kupitisha Azimio (Ibara 46A(10)) na kuweka Rekodi ya kuwa Rais wa Kwanza kuondolewa na Bunge kwa kujaribu kuichezea Demokrasia tunayoijenga kwa taabu na hatimaye apoteze Malipo yoyote ya Pensheni na Haki zingine (Ibara 46A(11)).

Kwa kuwa haki hii wamepewa Wabunge wa JMT na mimi si Mbunge, natumia fursa hii kwa mujibu wa Ibara ya 18(a) ya Katiba ya JMT kuwashauri wabunge wakaweke Historia hii mpya kwenye Kikao kijacho cha Bunge.

Eng. Mohamed M. Ngulangwa
Katibu wa Uadilifu Taifa
ACT-Wazalendo(0713417707)

Zitto Kabwe:''CCM wamdhibiti mwanachama wao MAGUFULI, wasipomdhibiti sisi Tutamdhibiti''


.......................
Zitto A mewasili
anasema hajui ni kwanini Polisi wamezuia Kongamano lao la Kuchambua Bajeti.

anasema
''juzi usiku siku ya jumaamosi, watu wetu wa usalama wa chama walinijulisha kwamba Jeshi la Polisi wananitafuta, wakaenda nyumbani kwangu na magari manne kunikamata bila kufuata utaratibu''

Zitto ''Jumanne iliyopita Kamishna Wambura alinipigia kuniomba nifike polisi''

Zitto ''Hii ya Jumaamosi walikuwa wanataka Kunivizia''

UPDATES
...................
Zitto ''Watu wetu wa Usalama wa Chama walihakikisha kwamba sitakamatwa ili niweze leo kupata fursa kuzungumza na watanzania kupitia nyie wana habari'

Zitto '' Hatufahamu Watawala wanaogopa nini mpaka kuzuia mikutano ya wanasiasa''

Zitto '' Nasikia Jana Walimkamata Mwenyekiti Mbowe wa Chadema Huko Mwanza kisa eti kawasalimia wananchi, huu ni uvunjwaji na ukiukwaji mkubwa wa utawala wa kidemokrasia''


UPDATES

Zitto ''Tunalaani tabia za KIDIKTETA za Rais Magufuli''

Zitto ''Magufuli ameanza na vyama vya siasa kuonyesha Udikteta wake, nawahakikishia akimalizana na Vyama vya siasa atahamia kwenu Wanahabari, Tumkatalie''

UPDATES

Zitto ''Ndio maana Magufuli Ziara yake ya Kwanza alifanya RWANDA, tumegundua kuwa alikwenda kujifunza namna ya Kudhibiti Demokrasia na Kuongoza Kidikteta''

Zitto '' Hauwezi kupamnana na UFISADI kama haumpi nguvu ya Kiutendaji wa CAG''

UPDATES
...................
ZITTO ''Kwa hali Hii anayokwenda MAGUFULI AJIANDAE KUWA RAIS WA TERM MOJA kwa sababu watanzania hawataweza kuvumilia kutawaliwa, kuminywa na kuburuzwa na Rais DIKTETA KAMA YEYE''

Zitto '' CCM wamdhibiti MAGUFULI, na wasipomdhibiti sisi na Watanzania Tutamdhibiti''

Zitto '' Hatutakaa Kimya hata kama atatufunga, akimfunga Zitto watazaliwa wakina Zitto wengine, na kwenye hili hatutakaa Kimya, tutasimama kidete mpaka nchi irudi kwenye misingi''

UPDATES
ZITTO ''IGP ameagizwa na MAGUFULI anikamate, lakini hawezi kunikamata bila kufuata utaratibu, hawawezi kunikamata kwa kunivizia, viongozi hatukamatwi kwa kuviwa viziwa, tumewaonyesha kwamba Polisi wanaweza klutukamata kwa kufuata terms zetu na sio zao''

UPDATES
ZITTO '' Karibuni kesho saa tisa kwenye Kongamano letu, Hatuwezi kuacha kufanya siasa, lazima tuendelee kufanya siasa, mmeudhuria mikutano yetu hamjaona hata sisimizi amekanyagwa''

UPDATES

Zitto '' Wanasema Bajeti imeongezeka kwa 32% ukweli ni kwamba Bajeti imeshuka kwa maana Dola imeporomoka''

UPDATES

ZITTO ''CCM wamdhibiti mwanachama wao MAGUFULI, wasipomdhibiti sisi Tutamdhibiti''

MASWALI

Jambo leo
Naomba unikumbushe sheria inayoruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano na makongamano

ZITTO ''Sheria ya Vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 inaruhusu vyama vya siasa kufanya siasa, makongamano na mikutano ni sehemu ya siasa, hatuhitaji kuomba kibali

SWALI
Je mkutano utarushwa Live


Zitto ''Tutaweka Utaratibu ili watanzania wengi zaidi waweze kushiriki kwenya kongamano'' 


 UPDATES
Zitto ''Polisi hawana mamlaka ya kisheria Kuzuia Mikutano ya vyama vya siasa, tunaipongeza Chadema kufungua kesi ya kikatiba mwanza, sisi tunafungua hapa Dar, na tunavitaka vyama vingine vifungue kesi ili ziwe nyingizaidi kudai haki''

UPDATES

Zitto ''Kama serikali haifanyi sawa sawa ni wajibu wetu kuwakosoa, na tutawakosoa tutawakosoa kama tulivyokuwa tukifanya serikali iliyopota...serikali ya sasa haina uvumilivu''

UPDATES
Zitto ''Bunge limenisimamisha Ubunge, tutatumia Forums nyingine kuwatetea wananchi na Demokrasia...Hatuhitaji kibali cha mtu yeyote kufanya kongamano''

SOURCE:Jamii Forums.

ZITTO KABWE:Serikali ya Magufuli Haipo Tayari Kukosolewa na Wapinzani Inatengeneza Mazingira ya Kuwanyamazisha

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo ameonya utawala wa Rais John Magufuli kuacha tabia ya kutaka kuziba midomo wapinzani.

Amesema, Serikali ya Rais Magufuli haipo tayari kukosolewa na wapinzani na kwamba, inatengeneza mazingira ya kuwanyamazisha sambamba na kuminya demokrasia.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema hayo leo baada ya kutoka kuhojiwa na Kamanda wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke na Naibu Kamanda wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa saa tatu.

“Mambo kama haya yalikuwa yanaanza kusahaulika katika mfumo wetu wa kisiasa nchi, lakini nyie ni mashahidi mnaona jinsi demokrasia inavyominywa na kuingia kwenye mashaka makubwa. Ni muhimu wananchi wakasimama kidete ili kuitetea demokrasia,” amesema Zitto na kuongeza;

“Wanatia woga wa watu kuzungumza mawazo yao ya kisiasa jambo ambalo si haki kwa kuwa ni sehemu ya wajibu wetu wa kisiasa. Hofu inayojengwa na serikali juu ya wanasiasa wa vyama vya upinzani haina maana.

“Kama leo polisi wametumia zaidi ya masaa matatu, hayo masaa waliyoyapoteza wangefanya kazi ya kupambana na majambazi, wahalifu na madawa ya kulevya badala ya kupoteza nusu siku kwa kutuhoji maswali,” amesema Zitto.

Anasema kuwa, ratiba ya kuzunguka mikoani itasitishwa kutokana na tamko lililotolewa jana na jeshi hilo.

Jeshi hilo limelizuia mikutano ya kisiasa hadi litakapotoa taarifa na kwamba, wanasheria wa ACT-Wazalendo  wataenda mahakamani ili kupata tafsiri sahihi.

“Lakini kama mnavyofahamu, jana limetolewa tamko la kuzuia mikutano yote hadi tamko lingine litakapotoka, hivyo basi tulikuwa tunashauriana na wanasheria ili wapate tafsiri ya kisheria kutoka mahakama kutokana na kwamba siyo sahihi polisi kuzuia mikutano.

“Lazima tuende mahakamani sababu bila ya kupata tafsiri ya mahakama, hatuwezi kufanya mikutano na hatutaki nchi iingie kwenye fujo,” amesema.

Steven Mwakibolwa, Mwanasheria wa ACT amesema kuwa, Zitto alihojiwa juu ya hotuba aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Jumapili wiki iliyopita na kwamba, yuko nje kwa dhamana isiyo na malipo.

“Tusubiri Jumatano wiki ijayo ili tujue kama atapelekwa mahakamani au upelelezi utajiridhisha kuwa hana makosa.

“Aliulizwa maswali mengi ambayo yalihusiana na hotu yake aliyotoa, amelezea kwa kina alichokisema maswali yote alijibu.”

Mwakibolwa amesema kuwa, kwa sasa si vema kueleza maswali aliyoulizwa kwa kuwa si muda na wakati sahihi wa kuliongelea suala hilo sababu liko chini ya upelelezi.

ACT- Wazalendo Wamteua Juma Saanani Kuwa Kaimu Katibu Mkuu


MAAZIMIO YA HALMASHAURI KUU YA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO KUFUATIA KIKAO CHAKE CHA

JUMATATU TAREHE 25 APRILI 2016


Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha ACT-Wazalendo ilifanya kikao chake cha kawaida jana (Jumatatu) tarehe 25 Aprili 2016 Jijini Dar es Salaam.


Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu:

1. Ilimteua Ndugu Juma Saanani kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Chama hadi pale uchaguzi mkuu wa ndani ya chama utakapofanyika.


Uteuzi huu unafuatia kung’atuka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Ndugu Samson Mwigamba anakwenda masomoni katika Chuo Kikuu cha Kenyatta.


Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Juma Saanani alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama (Zanzibar).


2.Ilipitisha Mpango Mkakati wa Chama utakaongoza programu za chama kwa kipindi cha miaka mitano (2016-2020).


3.Aidha, kwa kuzingatia mamlaka yake kikatiba (Ibara ya 29 (25iv), Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe (MB) amemteua Ndugu Samson Mwigamba kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Chama na Kamati Kuu imekwisharidhia uteuzi huo.


Uteuzi huu umefanyika kwa kuzingatia kuwa Mwenyekiti wa Kamati halazimika kufanya kazi makao makuu na hivyo Ndugu Mwigamba ataendelea na masomo yake bila kikwazo.


Ado Shaibu

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kuwa Umma.

Jumanne, 26 Aprili 2016.

ZITTO KABWE:SINA MPANGO WA KUMHUJUMU RAIS MAGUFULI



Kumekuwa na maneno yanasemwa na mimi kupuuza katika kipindi cha wiki kadhaa; kwamba ninapanga kumhujumu Rais Magufuli katika kazi zake. Maneno haya yanaenezwa na watu wanaotumwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Bwana Charles Kitwanga ( nina ushahidi usio na mashaka wa Kitwanga kupanga vijana wa wanaojiita wa UVCCM kufanya mikutano na waandishi wa habari na anawalipa fedha kufanya hivyo. Nataka ifahamike bila chenga kama ifuatavyo:

1) Ninamwunga mkono Rais katika kazi ya kusafisha Nchi. Hii ndio kazi nilikuwa nafanya katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Nitakuwa mtu wa ajabu sana nisipomwunga mkono Rais katika vita dhidi ya Ufisadi. Hata hivyo, kamwe sitasita kuweka wazi pale ninapoona Rais anafanya makosa. Na nimekuwa nikisema wazi wazi na kumkosoa Rais waziwazi. Lakini pia nimekuwa nikimwambia Rais kwa njia nyengine ambazo viongozi huwasiliana ninapoona anafanya sivyo. Kukosoa ni kazi moja muhimu sana na ya kizalendo kuliko lolote ambalo raia anaweza kufanya kwa kiongozi wake. Kukosoa Serikali ni uzalendo maradufu. Pale panapostahili nitapongeza. 

2) Namsihi Waziri Kitwanga amalize matatizo yake yeye mwenyewe. Yeye kama mmiliki wa Kampuni ya Infosys yenye mkataba na Serikali katika Wizara anayoongoza sasa anapaswa aone ni namna gani hana mgongano wa maslahi. Waziri Kitwanga asitafute watu wa kuwatupia lawama kwenye mambo yanayomhusu. Mimi binafsi sijawahi kugombana na Charles Kitwanga. Hajawahi kuwa rafiki yangu. Hajawahi kuni excite kama Kiongozi ( kimsingi nashangaa mtu kama yeye kuweza hata kuwa Waziri wa Wizara nyeti kama hiyo) . Zaidi ya yote Waziri Kitwanga sio 'size yangu'. Kwa protokali za Uongozi, size yangu mimi ni Rais Magufuli, bosi wake. Naanzaje kuhangaika na Kitwanga? Ili iweje? Namsihi asijipandishe chati kwamba mimi nataka kumtoa. Ningetaka kumtoa wala asingejua maana ningeshughulika na aliyemteua. Nasema haya sababu amekaa na Waziri Mkuu na Wabunge kadhaa akilalamika kuwa nataka kumtoa Uwaziri. Asinipe dhambi, Uwaziri atatolewa na aliyemteua kwa madhambi aliyofanya. Asitafute bangusilo! 

3) Mimi kwa wiki kadhaa sasa nipo nje ya Nchi ( nchini Marekani katika Chuo Harvard kwa masomo) . Sijui na sihusiki na njama zozote dhidi ya yeyote. Kwanza hizo sio aina ya siasa ninazofanya. Siasa ninazofanya ni Siasa za Maendeleo ya Wananchi na sio Siasa za kuwinda watu. 

4) licha ya kuwa Kiongozi wa Chama, Mimi ni Mbunge wa Chama Cha ACT Wazalendo. Kwa hiyo nafuata maelekezo ya chama changu katika kazi zangu. Chama changu katika Mpango Mkakati wake kimeniagiza kufanya Siasa za Maendeleo. Chama changu kinaunga mkono juhudi zote za Rais kurejesha imani ya wananchi kwa Serikali kwa kupambana na ufisadi. Hata hivyo Chama Cha ACT Wazalendo kinamtaka Rais ajenge mfumo imara wa kitaasisi ili mapambano dhidi ya ufisadi yawe endelevu. Hivyo, porojo za kwamba nataka kumwangusha Rais ni porojo za watu wasionijua binafsi na wasiojua misingi ya ACT Wazalendo 

5) Nawasihi Watanzania wote a) kumdharau Waziri Kitwanga na kumtaka ajibu tuhuma zinazomkabili za Kampuni yake binafsi kufanya kazi na Idara katika Wizara anayosimamia na kwamba ajipime kama anatosha kuendelea kumsaidia Rais kazi b) kuendelea kumwunga mkono Rais katika vita dhidi ya ufisadi. Kama nilivyosoma mwaka jana ' asiyemwunga mkono Magufuli yupo upande wa mafisadi' c) kuepuka siasa za porojo zinazoendeshwa na vijana wanaotafuta nafasi za kuteuliwa na d) kutaka umadhubuti wa kila jambo linasomewa ili kuepuka kuonea watu.

CHANZO:

ZITTO KABWE NDANI YA MKASI NA SALAMA JABIR

ZITTO KABWE:MAALIM AAPISHWE MARA MOJA



Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuhusiana na hali ya kisiasa Zanzibar,na haya ndio aliyoandika,,,

 
Suala la Zanzibar lisidharauliwe kabisa.Matokeo yatangazwe na mshindi aapishwe.Hatuwezi kutazama tu katiba inakanyagwa. Vinginevyo Maakim Seif apate Jaji amwapishe na aunde Serikali mara moja na kuanza kuwatumikia Wazanzibari,serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top