Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE MKUTANO WA TANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA NA CHINA, JIJINI JOHANNESBURG LEO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa China, Xi Jinping, wakati wa Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye kitambaa cheupe) akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye kitambaa cheupe katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika baada ya ufunguzi wa Mkutano huo Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi, walipokutana kwenye ufunguzi wa Mkutano huo Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Shulu Hassan, akisalimiana Mwambata wa Kijeshi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini (Defence advisor) Brig. Gen Ibrahim A. Kimario, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Olver Tambo jijini Johanesburg jana Desemba 3, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Shulu Hassan, akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Olver Tambo jijini Johannesburg jana Desemba 3, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China.
 Baadhi ya washiriki katika Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo leo jijini Johannesburg. 
Picha na OMR.

TASWIRA:MAKAMU WA RAIS MHE.SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA UONGOZI WA MTANDAO WA WANAWAKE TANZANIA.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Uongozi wa Mtandao wa Wanawake Tanzania (WFT) wakati viongozi hao walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Nov 24, 2015 kwa mazungumzo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea baadhi ya Vipeperushi na Vitabu vya Mtandano wa Wanawake Tanzania (WFT) kutoka kwa mwenyekiti wa mtandao huo, Prof.Ruth Meena, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dares Salaam, leo Nov 24, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mtandao wa Wanawake Tanzania (WFT) baada ya mazungumzo yao yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dares Salaam, leo Nov 24, 2015. 
Picha na OMR

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MAKAMU WA RAIS.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na uongozi wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania (WFT) ambapo amezungumzia dhamira ya serikali katika kuyatafutia ufumbuzi matatizo mbali mbali yanayowakabili wanawake na watoto wa kike nchini.

Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais aliueleza ujumbe huo kuwa wakati wa kampeni aliahidi pamoja na kazi za kumsaidia Mhe. Rais bado kama mama atafuatilia kwa karibu utekelezaji wa ahadi ya kupatikana kwa maji safi na salama, kuboresha afya ya mama na mtoto, elimu na mazingira.

“Nilipokuwa kwenye kampeni nimejionea shida ya maji na wanawake ndiyo wanaopata tabu ya kutembea mwendo mrefu kutafuta maji. Kwa hiyo, pamoja na kazi zangu za kumsaidia Mhe. Rais nitasimamia miradi yote ya maji, alau tuhakikishe maji yanapatikana umbali wa mita 400 kutoka eneo wananchi wanakoishi au karibu zaidi”.

Alisema kinachofurahisha zaidi suala la maji liko kwenye Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) na miradi mingi ikiwemo ya kuchimba visima virefu katika mikoa kama vile ya Singida na Dodoma iko kwenye mchakato na cha msingi ni kusimamia fedha zinatumika kuleta maji kama ilivyokusudiwa.

Kuhusu afya ya mama na mtoto alisema kazi hiyo ataianza hivi karibuni kwa kushirikiana na Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea haki za wanawake ili kupunguza vifo vinavyosababishwa na mimba za utotoni.

“Hili tutajitahidi kulipunguza kwa kiasi kikubwa na hasa baada ya serikali ya Awamu ya Nne kusema kwamba shule ya msingi ya lazima ni kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne”, alisema na kuongeza

“Katika kipindi hicho binti atakuwa amefikisha miaka 17, atakuwa tayari kukabiliana na mambo ya uzazi tofauti na ilivyo sasa ambapo anamaliza darasa la akiwa mdogo na matokeo yake anapata mimba katika umri mdogo. Mtusaidie kupiga debe huko nje utekelezaji uweze kufanikiwa.”

Hata hivyo, alisisitiza kusimamia suala la kuhakikisha zahanati, vituo vya afya na hospitali nchini zinakuwa na dawa na vifaa tiba vya kutosha katika wodi za wazazi kwa ajili ya kuhudumia akina mama na wananchi kwa ujumla ambao wengi wanaonekana ni watiifu kwa serikali yao.

Kwa upande wa elimu Mhe. Samia alisema atasimamia ujenzi wa mabweni kwa watoto wa kike na kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwa sababu uharibifu wa mazingira ndiyo umekuwa chanzo cha upungufu wa maji nchini.

Aidha aliuambia ujumbe huo kuwa hivi sasa tuna mpango wa kuimarisha utendaji serikalini kuanzia serikali kuu hadi serikali za mitaa ili kinachopatikana kidogo kimfikie kila mwananchi.

“Tutaendelea kuaihirisha sherehe ili fedha hizo ziweze kutumika kwa mambo ya kijamii. Kwa msimamo huu amabao Mhe. Rais ameanza nao labda watu wote tushirikiane kwa kutatua matatizo yetu kwa gharama nafuu kwa ufanisi mkubwa.”

Mapema akizungumza kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti wa Mtandao huo Prof Ruth Meena alimpongeza Mhe. Samia kwa kushika nafasi ya juu ya uongozi akiwa mwanamke wa kwanza kuweka historia katika Tanzania.
Alimweleza Mhe. Makamu wa Rais matarajio yao kwa serikali ya Awamu ya Tano kuwa itatetea misingi ya haki na usawa katika Nyanja zote.

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
24/11/2015.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA DINI WA MKOA WA DODOMA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, wakati alipokutana nao kwa mazungumzo kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo Nov 16, 2015. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa (kulia) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, Sheikh Ahmad Said Ahmed. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,  Chiku Galawa, wakati wa mkutano na Viongozi wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo Nov 16, 2015. Picha na OMR
Baadhi ya Viongozi wa Dini wa Mkoa wa Dodoma,wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, wakati akihutubia alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma, leo Nov 16, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, wakati alipokutana nao kwa mazungumzo kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo Nov 16, 2015. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Chiku Gallawa (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, Sheikh Ahmad Said Ahmed, kwa pamoja wakisimama kuomba dua wakati wa mkutano na Viongozi wa Kamati hiyo,mkoani Dodoma leo, Nov 16, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, baada ya kuzungumza nao kwenye mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo, mjini Dodoma leo Nov 16, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, baada ya mkutano uliofanyika leo Nov 16, 2015 kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, baada ya mkutano uliofanyika leo Nov 16, 2015 kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, baada ya mkutano uliofanyika leo Nov 16, 2015 kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Picha na OMR
makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, Askofu wa Kanisa la KKKT Mkoa wa Dodoma, Kinyunyu Amon, baada ya mkutano uliofanyika leo Nov 16, 2015 kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Picha na OMR

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA ASHIRIKI HAFLA YA DUA YA KUOMBEA TAIFA AMANI, JIJINI DAR


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akihutubia wakati wa hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akishiriki dua ya pamoja na baadhi ya viongozi, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani Tanzania, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jana Nov 7 2015. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Agape Television Network (ATN) Dkt. Anny Fernandes, wakati wa  hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR
 Baadhi ya Viongozi waliohudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Makamu wa Rais Mama Samia, alipokuwa akihutubia. Picha na OMR
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Agape Television Network (ATN) Dkt. Anny Fernandes, wakati wa  hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa, akizungumza wakati wa hafla hiyo, alipokuwa akiomba dua maalumu. Picha na OMR
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jana. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akiagana na baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla ya kuliombea Taifa amani wakati akiondoka ukumbini baada ya kuhutubia katika hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Kamanda Suleiman Kova, wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kwa ajili ya kuhudhuria hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Libelata Mulamula, wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kwa ajili ya kuhudhuria hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani, jijini Dar es Salaam jana Nov 7, 2015. Picha na OMR
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top