Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Buguruni Jana jioni Machinga wawapo mzigoni

Wanaonekana watu wengi wakipita pembezoni mwa barabara kutokana na eneo la waendao kwa miguu kugeuzwa sehemu ya kufanyia biashara muda wa jioni.
Wakiwa wanapita eneo linalotenganisha barabara ambalo hupandwa nyasi na miti ili kupendezesha mandhari ya mji hii ni kutokana na msongamano unaotokea pale wamachinga wanapoingia mzigoni mida ya jioni.

Hii ni Buguruni jioni ya jana ambapo muda wa jioni hujaa shughuli na heka heka kutokana na wafanyabiashara ndogondogo ''machinga'' huligeuza eneo hilo lote kuwa sehemu ya kufanyia biashara hivyo hata wapita njia kuwa na wakati mgomo kupita eneo hilo kama inavyonekana katika picha nilizo kutumia ambapo inatubidi wapita njia tupite pembezoni mwa barabara au katikati ya barabara hizo mbili kitendo ambacho kinahatarisha usalama wetu tupitapo hapo.Elewa kuwa eneo hilo hushuka watu wengi toka maeneo mbalimbali ya mji kuna wanatoka Muhimbili,Kariakoo,Msasani,kawe na maeneo mengine acha wanaokuja sokoni

Buguruni na kuelekea maeneo mbalimbali ya jiji Kama Gongo la Mboto,Mbagala,Tabata naUbungo nk.

Nimekupa hii labda mamlaka husika zitaona Mbona Ubungo iliwezekana hapa shida ni nini ?

Mdau wako(Rundugai blog)

Andrew Alex

(E mail imewekwa kapuni kwa sasa)

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top