Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

KUTOKA BUNGENI :Mgomo wa Madaktari nchini Mbunge awanyooshea kidole CHADEMA



Mbunge Mh.Eng.Stella Manyanya leo Bungeni akichangia Bajeti ya Ofisi ya Rais amekishutumu chama cha demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kuhusiana na mgomo unaoendelea wa Madaktari kuwa wana la kujibu hapo


"CHADEMA mnalo la kujibu.Ninyi ndiyo mnaofanya mgomo wa madaktari uendelee"-MH.Manyanya.


Baada ya maneno hayo Mh.J.Mnyika aliomba muongozo wa Mwenyekiti

akisema 'Mimi ni kiongozi wa Chama.Hayo anayozungu.....''


kabla ya kumalizia alichokuwa anataka akaamriwa na Kiti.''Kaaa chini''


Akaendelea baada ya ruhusa ya Kiti...

"Mimi ni Mbunge,ni kiongozi wa chama.Nashiriki katika vikao vyote vya chama.Jambo kuwa CHADEMA linahusika si kweli''

Akaongeza kuwa

''Naomba taarifa rasmi ya Kamati ya Afya ije rasmi bungeni."

"Naomba aliyetoa tuhuma CHADEMA inahusika na migomo wa madaktari athibitishe''

Baada ya hapo akapewa nafasi Mh.Mwigula akasema ...

''Hawa wanaleta kimbele mbele CHADEMA.Dr.Ulimboka ni nani kwao?"-


Baada ya kuingilia Mh.Mwigula alisema hata hotuba zao zinaonyesha kuwa wanahusikahao.

Hali hiyo ilimuinua Mh.Mnyika ambae alikalishwa chini na Mwenyekiti alimuambia nimesema kaa chini unawashwa washwa eeh hapo''


Hali iliyomsikitisha mno Mh.Mnyika ambae alionekana kupitia Luninga akitabasamu huku akitikisa kichwa kuonekana kutopendezwa na kauli hiyo.


Kutokana na Malumbano hayo Mh.Stella Manyanya alipewa nafasi kuendelea huku Mwenyekiti akisema Mh.Mnyika ameshindwa jibu hoja ya Mh.Mwigula

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top