Kutoka Bungeni muda huu wakati mbunge wa Mbeya Mjini Mh.Joseph Mbilinyi akichangia jioni hii.Malumbano hayo yalizuka kati ya mwenyekiti anaeongoza bunge muda huu na Mh.Mbilinyi huku Mh.Lissu akitaka kutoa taarifa na kukataliwa .
Mh.mbilinyi aliaanza kusema kwa kuwashangaa wabunge vijana wa CCM kuwa wamekuwa hawawaambii ukweli wazee wao kuwa ni nini kinaendela mtaani na wamekaa wakiwazia na wanawazi uwaziri,ukuu wa wilayana ukuu wa Mkoa.
Pia anashangazwa na wabunge hao kusimama bungeni na kumpongeza Rais kwa kuteua wakuu wa Wilaya wakati wanajua fika ile ni mojawapo ya majukumu ya Rais.Akasema kuwa ipo siku mtampongeza kwa yeye kunywa maji.
Kazi alianzia pale Mh.Mbilinyi alipoanza kuzungumzia suala la Kutekwana kutesa kwa Dr.Ulimboka kuwa kumezukahali ya ajabu nchini kwani suala hilo ni mtiririko wa matikio yaliyowakuta wabunge wa CHADEMA Mh.Kiwia na Mh.Machemli pale walipopigwa kule Mwanza.Anashangaa utamaduni huu umezuka wapi wa kung'oa watu meno na kucha akiitaka serikali kuangalia hali hii isiendelee.akatoa mfano wa Rais wa Sudan Bashir kuwa alishitakiwa mahakama ya kimataifa(ICC) sio kwamba wanajeshi na Polisi ndio waliokuwa wanatesa watu bali ni kikundi cha Janjaweed ndicho kilichokuwa kinafanya hayo yote.
"Kama suala la kutekwa na kuteswa kwa Dr.Ulimboka nina uhakika nalo, na kila mtanzania ana uhakika nao"-Mh.Mbilinyi
hapo akasimama Mh.Mary Nagu kuomba muongozo wa Mwenyekiti kwa mujibu wa kanuni kifungu cha 64(1)a ..akamtaka Mh.Mbilinyi aamriwe adhibitishe kuwa serikali inatumia Janja weed kumteka na kumtesa Dr.Ulimboka.
Alipoamriwa kufuta kauli yake Mh.Lissu alisimama akisema taarifa Mh.mwenyekiti lakaini akamriwa akae chini Mh.Lissu akaogoma akisema unajua nataka kuongea nini mpaka unaniamru kukaa chni ?
Mh.Mwenyekiti akasisitiza kaa chini.
Mwenyekit akamuambia Mh.Lissu kuwa natafuta umaarufu.
''Usitake cheap popularity hapa. Usitake umaarufu hapa Lissu"-
"Suala la Ulimboka lisiendelee kujadiliwa"-Kiti cha Spika
Mh.Mwenyekiti akampa nafasi Mh.mbilinyi ambae alisema wamemnukuu sivyo kwani yeye alitoa Mfano kuhusu janja weed hivyo akaendelea kutoa mchango wake kwenye Bajeti Ofisi ya Rais.
Loading...
Chediel . Powered by Blogger.
Post a Comment