Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Marekani yaipa Kenya ndege za kisasa


Taarifa kutoka Marekani zinaeleza kuwa Wizara ya Ulinzi ya
Marekani itaipatia Kenya ndege nane ndogo zisizohitaji rubani, ikiwa ni sehemu
ya msaada wa kijeshi kwa nchi za Afrika Mashariki, ili kuzisaidia kupambana na
wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia, al-Shabaab.



Gazeti la Wall Street Journal la Marekani limearifu kuwa Kenya itapata ndege
hizo ambazo hazitakuwa na silaha, lakini zinaweza kugundua maeneo yanayofaa
kulengwa na ndege au majeshi ya ardhini.



Gazeti hilo limesema ndege zisizokuwa na rubani ni sehemu ya msaada wa
Marekani, pamoja na malori, zana za mawasiliano, na silaha kwa Burundi, Djibouti
na Uganda.


Chanzo:http://www.bbc.co.uk/swahili
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top