Wafuasi wa Mombasa Republican Council wakishangilia
Mahakama moja mjini Mombasa imeondoa marufuku iliyowekea vuguvugu la Mombasa Republican Council.
Mombasa Republican Council( MRC) ni vuguvugu lililoanzishwa na wenyeji wa Pwani ya Kenya wakitaka eneo hilo la Pwani lijitenge na Kenya na kuwa nchi huru.
Mahakama hiyo imesema kuwa kundi hilo ambalo makao yake makuu ni mjini Mombasa sio kundi la kifalifu bali linaendesha harakati za kisiasa.
katika uamuzi wake jopo la majaji watatu walishauri kundi hilo kujisajili rasmi kama chama cha kisiasa.
Serikali ilikipiga marufuku kikundi hicho cha MRC mwaka wa 2010, ikisema kuwa kundi hilo ni la kihalifu.
Lakini Serikali imetangaza kuwa itakata rufaa kupinga uamuzi huo likidai kuwa ni kinyume na katiba ya Kenya.
Wadadisi wa maswala ya kisiasa wanasema kuwa uamuzi huo wa mahakama utalipa kundi hilo nguvu ya kuendeleza harakati zake za kutaka kujitenga kutoka Kenya.
Kuna hofu kuwa hali hii itatatiza uthabiti wa kisiasa nchini Kenya.
Kundi hilo la MRC limekuwa likiilaumu serikali kwa madai ya kuwa nyanyasa wakaazi wa pwani na kulitelekeza jimbo hilo zima.
Wakuu wa MRC pia wamekuwa wakisema hawaoni faida kutokana na rasilmali zilizoko pwani.
Kutokana na harakati zao wasuasi wengi wa MRC wamekuwa wakikawatwa na kushitakiwa kwa kuwa wanachama wa kundi haramu.
Baada ya mahakama kutoa uamuzi wa kulindolea kundi hilo marufuku iliyowekwa na serikali , sasa haijulikani kama serikali itaondoa kesi za watu walioshitakiwa.
Chanzo:BBC Swahili
Post a Comment