Kikosi cha Mabingwa Watetezi Kagame Cup 2012
YANGA imeingia Fainali baada ya kupata ushindi wa Goli moja kwa bila dhidi ya APR sasa kukutana uso kwa uso na AZAM katika Fainali inayotazamiwa kuwa kali na ya kukata na Shoka kutokana na wababe hao Azam kuwaondoa Simba katika Robo Fainali hivyo kutaka kuwadhihirishia Yanga kuwa wao ni Kiboko ya Vigogo nchini.
Dakika 30 za nyongeza Yanga 1-0 APR FT
Dakika ya 27:APR wanajitahidi kusukuma mashambulizi lakini Yanga wako imara kuosha hatari zote
Dakika ya 10 Hamis Kiiza anawainua mashabiki wa Yanga kwa kupachika bao la kwanza, ni baada ya kumalizika kwa dakika tisini, na kuongezwa kwa dakika 30
Baada ya kutoka sare ya 0 - 0 katika dakika 90 Mchezo umeongezwa dakika 30
Dakika ya 90 za mchezo zimemalizika, Young Africans 0 - 0 APR
Dakika ya 86, Young Africans inafanya mabadiliko anaingia Rashid Gumbo anatoka Shamte Ally
Dakika ya 85: Yanga (Tanzania) 0 - 0 APR (Rwanda)
Dakika ya 80: Yanga 0-0 APR
YANGA WAMECHARUKA dakika ya 76
Dakika ya 71: Yanga (Tanzania) 0 - 0 APR (Rwanda)
Milango bado migumu uwanja wa Taifa, Si Yanga si APR
Dakika ya 66, Said Bahanunzi anakosa bao la wazi
Dakika ya 60, Young Africans 0 -0 APR
Kipindi cha pili cha mchezo ndio kimeanza, Young Africans 0 -0 APR
Half Time: Yanga 0-0 APR
DaKika ya 42: YANGA O - 0 APR
Dakika 40: Yanga 0-0 APR
Hamis Kiiza na Godfrey Taita wamepata kadi za njano dakika ya 38
Dakika ya 33 YANGA 0 APR 0
Dakika ya 30, Young Africans 0 - 0 APR
Dakika ya 26, Young Africans inafanya mabadiliko anaingia Shamte Ally anatoka Juma Abdul
Dakika 20: Bado timu zinacheza kwa kushambuliana na hakuna iliyokwisha ona goli la mwenzake
Dakika ya 15, Young Africans 0 - 0 APR
Mpira ndio umeanza hapa uwanja wa Taifa - Nusu Fainali kati ya Young Africans Vs APR
YANGA wameanza hivi:
1.Ally Mustapha 'Barthez' - 1
2.Juma Abdul - 14
3.Oscar Joshua - 4
4.Nadir Haroub 'Cannavaro' (C) - 23
5.Kelvin Yondan - 5
6.Athuman Idd 'Chuji' - 24
7.Godfrey Taita - 17
8.Haruna Niyonzima - 8
9.Said Bahanunzi - 11
10.Hamis Kiiza 'Diego' - 20
11.David Luhende - 29
Post a Comment