Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Rundugai na Kawaya zatoka sare katika mpambano wa kukata na shoka.

Mpira wa Miguu umekuwa ni mchzeo unaopendwa sana kila sehemu hapa nchini iwe mijini au vijijini hutakosa kosa ona kiwanja kwaajili ya mchezo huo hata kama ni duni kiasi gani Lazima wadau hao wa mchezo huo watakuwapo.Huchangishana ili waweze angalau nunua jezi au mpira ili waweze kuwa na timu yao na mara kwa mara hualikana kucheza mechi za kirafiki.

Hapo juu ni baadhi ya wachezaji wa timu ya mpira wa miguu wa timu ya Rundugai wakipasha kabla ya mechi yao na Timu ya Kawaya katika mechi iliyoishia kwa sare ya bila kufungana. Katika mpambano huo mechi hiyo huwa ya mshikemshike kutokana na majirani hao kutambiana kila wakutanapo.

Rundugai ikiwa na wachezaji mahiri kama Abdu,Stephano,Ombeni ,Omary ambao waliliandama lango la Kawaya mara kwamara katika uwanjawao huo wa nyumbani lakini walishindwa tumbukiza mpira kwenye kamba.

Timu hiyo hucheza mechi za mujirani mwema na timu za Mbatakero,Boma na Kia mipambano inayojaa shamrashamra za kila aina.

Ni jukumu la wadau mbalimbali kuweza kusaidia vijana kama hawa ili kunyanyua mchezo huo wampira wamiguu.


Habarina Picha na Mdau wa Rundugai Blog
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top