



Kocha Sir Alex Fergurson ameweka wazi kuwa msimu huu wa EPL washindani wao wakubwa ni Chelsea kutokana na timu hiyo kuchukua Ubingwa wa Klabu Bingwa ya Ulaya.
Anasema kuwa Roman alikuwa na hamu sana na Ubingwa huo na ameupata hivyo itakuwa chachu kubwa sana kwa timu hiyo kuendeleza makali yao ili waweze kuchukua tena Ubingwa wa EPL 2012/2013.
Pia Chelsea wamefanya usajili mzuri msimu huu kwa kuwachukua Mjerumani Marko Marin na Mbeligiji Eden Hazard hivyo timu hiyo imeimarika.
Hata hivyo amesema timu yake iko imara kurudisha heshima yake na wako tayari kwa mapambano.
Hapo keshowanakutana uso kwa uso na Drogba na Anelka na timu nzima ya Shanghai SHenhua.
Post a Comment