Golikipa wa Police Kota akifuatilia kwa makini jinsi mpambano unavyoendelea akiwa na jezi ya mchezaji wa Arsenal Arshavin Beki wa Polisi Kota kulia akiangalia kwa makini mpira uliokuwa unatoka nje ili mpinzani wake asiupate na kuleta madhara golini mwake. Mshambuliaji wa Reminati Fc akitabasamu baada ya kupigiwa filimbi na refa kuwa ameotea hivyo kutoa tabasamu kali kwa golikipa wa Polisi baada ya kubaki wao wawili kabla ya filimbi.
Beki akiwa anaangalia mpira wa kona unaoelekea golini mwake Kama ilivyo kawaida ya viwanja vyetu wapita njia nao wakikatiza Kona hiyo ikielekea golini mwa Polisi Kota na Kapten(jezi namba 9) akiwa makini na golikipa wake akiwa tayari kuucheza mpira huo. Baadhi ya Mashabiki wakiwa wamekaa pembeni mwa Shule ya Msingi Tabata wakifuatilia kwa makini mpambano huo kati ya Reminati Fc vijana wa Tabata Bima na Police Kota wakimenyana.
Post a Comment