Uhispania wameweka historia kwa kuibugiza Italia magoli 4-0 katika Fainali ya euro 2012 mchezo uliochezwa jana Usiku mjini Kieve,Ukraine.
Pamoja na Italia kujitahidi kuwadhibiti Uhispania lakini jitihada zao zilishindwa na kujikuta wakiangukia mikononi mwa Wahispania hao waliokuwa wakicheza kandanda maridadi ambalo kilammojaanakubali kuwa kwa sasa ndio timu bora zaidi duniani.
Kocha Vicente del Bosque wa Uhispania pia ameweza kuweka rekodi ya kuwa Kocha alieweza kutwaa mataji maarufu duniani(soma hapa).
Alikuwa ni David silva alieunganisha kwa kichwa krosi karibu kabisa na goli kuipatia timu yake goli la kwanza kunako dakika ya 14 ya mchezo kabla ya mchezaji mpya wa Barcelona Jordi Alba kutumbukiza kwenye kamba goli la pili dakika ya 41 ikiwa pia ni katika kipindi hicho cha kwanza akimalizia pasi maridadi kabisa aliyopenyezewa.
Kipindi cha pili kilianza kwa Italia kujitahidi kuwazuia Uhispania kuongeza magoli lakini jitihada zao hizo zilipata pigo baada ya mchezaji wao Thiago Motta aliejeruhiwa kutoka njee hivyo kulazimika kucheza pungufu ya mchezaji mmoja,hivyo kuipa mwanya Uhispania kuutawala mchezo huo kaBISA na ilikuwa ni dhahiri kuwa lilikuwa ni suala la muda tu kwa Italia kupigwa goli zaidi.
Mchezaji anaerudisha makali yake kwa sasa Fernando Torres aliingia na katika mpira wake wa kwanza kupiga ni pasi maridadi aliyoimalizia na kuwa goli la tatu katika dakika ya 84 na yeye kuweza kuwa mchezaji ambae ameweza kufunga kwenye Fainali mbili mfululizo.Huku wakiaanza sasa kushangilia Ubingwa huo alikuwa ni Mata tena alitokea benchi kuipatia Uhispania goli la nne dakika ya 88 hivyo mpaka dakika ya mwisho Uhispania kuwa Mabingwa tena wa EURO 2012.
Kocha wa Italia Cesare Prandelli pamoja na kipigo hicho toka kwa Uhispani alazimaajivunie kikosi chake kutokana na kiwango walichoonyesha katika mashindano hayo.
Picha Na Daily Mail
Habari;Chediel
Post a Comment