Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WAUMINI WAFUNGA LANGO LA KUINGILIA KANISA KUU LA KKKT IRINGA, LENGO NI KUSHINIKIZA ASKOFU WA DAYOSISI YA KKKT IRINGA DK MDEGELLA AACHIE NGAZI


Hili ndio Kanisa Kuu la KKKT dayosisi ya Iringa
Huyu ndio Lawrenace Mtatifikolo aliyefunga kanisa hili leo jumapili ili waumini
wasifanye ibada. lengo lake ni kushinikiza mabadiliko ya uongozi ndani ya
Dayosisi ya KKKT Iringa

huyu ni Mchungaji wa Kanisa hilo, Mchungaji Huruma Bimbiga
JESHI la Polisi limemkamata na kumuhoji Lawrence Mtatifikolo (30) anayetuhumiwa kufunga kwa minyororo na makufuli mageti ya kuingilia Kanisa Kuu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Iringa.

Mtatifikilo alifanya tukio hilo jana majira ya saa 11 asubuhi ikiwa ni masaa mawili kabla misa ya kwanza katika kanisa hilo, haijaanza.
Katika mahojiano na waandishi wa habari kanisani hapo jana, Mlinzi wa kanisa hilo Anderson Mgoba alisema Mtatifikolo akiwa na wenzake watatu walifika katika lango kuu la kuingilia katika kanisa hilo majira ya saa 11.00 asubuhi.

Alisema baada ya kufika katika lango hilo, yeye pamoja na walinzi wenzake hawakuwa na shaka nao kwasababu ndani ya uzio wa kanisa hilo wanaendesha biashara ya kupaki magari.

“Walipofika tulidhani ni madereva wa magari yaliyokuwemo ndani ya uzio wa kanisa hili, hata
hivyo katika mazingira ya kushangaza walitoa minyororo na kuanza kufunga lango hilo kuu la kuingilia ndani,” alisema.

Alisema walitumia mnyororo na kufuli mbili kufunga lango hilo na kutoweka katika eneo
hilo kabla Mtatifikolo ajarejea tena na kudai apewe kufuli zake na mnyororo baada ya yeye kwa kushirikiana na walinzi wenzake kubomoa kufuli mbili zilizotumika kufunga lango hilo kwa kutumia tindo.

“Alipokuja kudai mnyororo na makufuli yake ndipo tulipomkamata na kumpeleka kituo cha Polisi cha kati kilicho jirani kabisa na kanisa hili,” alisema ana kuthibitisha kwamba amefanya mahojiano na Polisi na kuwapa taarifa hiyo.

Akikiri kutokea kwa tukio hilo, Mchungaji wa Usharika huo, Huruma Bimbiga alisema hawajui sababu za vijana hao kufunga milango ya kanisa hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanyiwa mahojiano na Polisi jana, Mtafikilo aliyeachiwa huru baada ya kupata dhamana alisema ahofii uamuzi alioufanya kwa kuwa unalenga kuinusuru KKKT Dayosisi ya Iringa inayokabiliwa na migogoro mikubwa ya kimaadili na kiuongozi.

“Siujutii uamuzi wangu huu, nimeamua kujitoa muhanga kwa niaba ya waumini wengine lakini si kwa lengo la kuwazuia waumini wa Dayosis hii kuabudu, lengo langu ni kuhakikisha
Dayosisi yetu inakuwa na viongozi wanaofuata maadili,” alisema na kuongeza kwamba wamechoshwa na uongozi wa mabavu na usiofuata maadili wa Askofu wa
Dayosisi hiyo Dk Owdenberg Mdegella.

Alisema yeye kwa kushirikiana na waumini wenzake wanne (hawakuwataja majina) walifunga safari kutoka usharika la Balali kata ya Image wilayani Kilolo na kwenda kulifunga
kanisa hilo kuu ili kufikisha ujumbe kwa Askofu huyo kwamba anatakiwa kujiuzulu nafasi yake hiyo.

Akitakiwa kutoa ufafanuzi juu ya madai hayo, Dk Mdegella alisema hawezi kuzungumzia suala lililotokea katika usharika mmoja huku yeye akiwa ni kiongozi wa makanisa yote ya Dayosisi hiyo.

Pamoja na kuguswa moja kwa moja katika tukio hilo, Askofu Mdegella alisema kwa njia simu
kwamba hana taarifa za kanisa kuu kufungwa minyororo na makufuli na kwamba
waliofanya hivyo walilenga kufikisha ujumbe kwake.

“Kwanza mimi niko safarini naelekea Dodoma, na kwa kuwa mimi ni kiongozi wa makanisa ya
dayosisi nzima, siwezi kuzungumzia suala hilo, wafuateni viongozi wa kanisa watawaeleza,” alisema na kuongeza Mungu ambariki mwandishi wa habari hii kwa kumpigia simu.

Kaimu Kamanda wa Polisi, Peter Kakamba aliahidi kutoa taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo kesho jumatatu.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top