Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

ALIETAKA KUJINYONGA HADHARANI HUKO IRINGA SASA ATAKA KUCHEZA MUZIKI MBELE YA HADHARA UWANJA WA SAMORA

Aliyekuwa mfanyabiashara maarufu Ramadan Mrisho Kasawa a.k.a Makosa akiwa katika ofisi za klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) kubadili wazo lake la awali la kujinyonga sasa adai atajinyonga nyonga kwa kucheza muziki katika uwanja wa Samora


Siku chache baada ya aliyekuwa mfanyabiashara maarufu mkoani Iringa Ramadhan Mrisho Kasawa "Makosa" kutangaza katika vyombo mbali mbali vya habari ukiwemo mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa anategemea kuandaa tamasha kubwa katika uwanja wa samora kwa ajili ya kujinyonga kwa kiingilio na fedha hizo kutumika kusaidia yatima leo ameibuka tena na kukanusha wazo lake hilo na sasa amedai atafanya onyesho kwa ajili ya kucheza muziki (kujinyonga nyonga ) na fedha hizo kusaidia yatima na kuendesha maisha yake .


Pia alisema kiasi cha fedha atachangia elimu kwa kununua madawati katika shule mbali mbali za msingi kulingana na mwitikio wa watu watakaofika katika tamasha hilo.


Huku akidai kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo atakuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Terresia Mahongo na kuomba wadau mbali mbali wakiwemo wafanyabiashara kujitokeza kumdhamini katika tamasha hilo kubwa .


Alisema lengo la kufika kubadili wazo hilo limekuja baada ya kupokea maoni ya wadau wengi kutoka pande mbali mbali za dunia wakimtaka asijinyonge na badala yake kufanya jambo jingine la kihistoria.


Makosa amepata kuwa mfanyabiashara mkubwa mkoani Iringa akiwa ni mmiliki wa mabasi ya abiria ,kumiliki Hospitali ya makosa , bendi ya Muziki Makosa Hoteli pia ndie aliyejitolea kupanda miti katika mji wa Iringa 
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

2 comments

HAKUNA KIONGOZI WA IRINGA YEYOTE ATAKAYE FIKIA HISTORIA HIYO YA MAKOSA KWASABABAU WOOOTE NI WABINAFSI! WANATAFUTA UMAARUFU KWA AJILI YA KUJINEEMESHA KISIASA TU KUPITIA MISAADA WANAYODAI WANAITOA UNAFIKI MTUPU!!!!!SRY KWA NENO HILO!!!

Reply

kweli jamaa huyu alijitolea sana hasa kupanda miti mjini hapa mpaka leo sijui kuna mtu yeyote alieweza hilo

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top