Shule hii ipo wilayani Muleba mkoani Kagera. |
Ndani ya shule hii licha kuwa ni shule yenye kuta na kuezekwa kwa nyasi, bali pia wanafunzi wanakaa chini |
Hali ya elimu imezidi kuwa mbaya kila kukicha, kiasi kwamba hata watu hudiriki kuuliza kama shule hizo zipo nchini, hasa wakiangalia juhudi na kelele nyingi zilizopigwa juu ya mchango mkubwa wa MMEM na MMES kuwa zimefanya kazi kubwa sana kuboresha mazingira ya kujifunzia hasa miundombinu ya shule.Swali Je, shule hizi ziliachwa wapi na mipango hii? Je bajeti ya elimu ya 2012/2013 itatatua baadhi ya changamoto za elimu nchini?na kuondokana na majengo haya yasiyo rafiki kwa mwanafunzi na mwalimu?
Mwana blog ya HakiElimu, Hebu angalia jinsi ambavyo wanafunzi huko Tanga,Rukwa,Kagera na Ruvuma wanavyojifunza kwenyesehemu zinazokatisha tamaa : Watatoka?
Na Hakielimu Blog.
Post a Comment