Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Maasai akilipa nauli ya Boda boda

KIJANA wa Kimasai, akimlipa nauli mwendesha pikipiki baada ya kufikishwa eneo la Kawe Kanisani jijini Dar es Salaam, leo mida ya mchana. Kilichonivutia zaidi ni namna alivyosheheni 'zana' kiunoni, wewe unasemaje mdau? 
 
Pikipiki maarufu kama bodaboda zimeweza kushika kasi kubwa nchini kutokana na kuweza kurahisha watu wa rika mbalimbali kuweza kuutumia kwa urahisi wa bei.
 
Pamoja na urahisi huo usafiri huo umekumbana na lawama lukuki kutokana na waendeshaji wa vyombo hivyo kutoweza kuzingatia sheria za usalama barabarani.Hivyo kusababisha vifo vingi nchini kwa mujibu wa taarifa ya  Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani (taarifa ya Jan-Feb 2011 na Jan-Feb 2012) ajali za pikipiki zimepungua kwa 22% lakini vifo vikiongezeka kwa 19% na mikoa 10 ambayo ina ajali nyingi za pikipiki ni Pamoja na Mkoa wa Dar Es salaam unaongoza ikifuatiwa na Morogoro, Ruvuma, Arusha, Pwani Mwanza, Tabora, Kilimanjaro, Manyara na Mtwara.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top