Mgeni rasmi mkuu wa Wilaya ya Iringa Dkt Leticia Warioba akisoma risala mbele ya makarani wa sensa waliofuzu mafunzo yao.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Bi Theresia Mahongo akisisitiza jambi kabla ya kumkaribiasha mgeni Rasmi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Bi Theresia Mahongo akisisitiza jambi kabla ya kumkaribiasha mgeni Rasmi.
.........................................
Zaidi
ya Makarani 260 watakaoshiriki zoezi la sensa ya watu na makazi
Manispaa ya Iringa mjini wametakiwa kutenda kazi hiyo kwa moyo na
uaminifu mkubwa kama mafunzo yanavyosema ili taarifa zinazohitajika na
serikali kupitia zoezi hilo la sensa ziweze kufanikiwa.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya makarani wa sensa yaliyoendeshwa kwa muda wa wiki mbili Katika Manispaa ya Iringa Mjini,
Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Leticia Warioba amesema anaamini makarani hao
walipatiwa mafunzo yao ipasavyo kama wakufunzi walivyowafundisha mafunzo
hayo na kusema wao wanategemewa kwa kiasi kikubwa kufanikisha zoezi
hilo ambapo serikali imedhamiria kukusanya takwimu ya watu na makazi
ifikapo tarehe 26 August ikiwa ni moja ya vipaumbele vya taifa.
Ameongeza
kuwa madhumuni makubwa ya mafunzo hayo yalikuwa ni kuwawezesha na
makarani na wadadisi ili waweze kukusanya takwimu sahihi. Amesema endapo
watakiuka mafunzo waliyopatiwa kutapelekea zoezi hilo kutofanikiwa hali
ambayo haitegemewi na yeye pamoja na serikali kwa ujumla hivyo
wanatakiwa kutambua dhamana waliyokabidhiwa ni kubwa hivyo ni azima
waifanye kama inavyotakiwa.
Pia
amewataka kupambana na changamoto zitakazojitokeza na kuhakikisha
wanatoa taarifa mapema kwa wasimamizi wao mara moja pindi wanapokutana
na changamoto ili ziweze kutatuliwa haraka na zoezi la sensa liendelee.
Amewataka
viongozi wa dini, siasa na wananchi kutoa ushirikiano katika
kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hili la sensa.
Nakuwaomba wananchi kutunza kumbukumbu zote za taarifa za maswali
yatakayoulizwa kwa wale watu waliolala katika kaya zao usiku wa kuamkia
tarehe 26 Augusti mwaka huu. Nakuwataka wale ambao wana wake wengi kwa
maana ya mkuu wa kaya kutoa taarifa sahihi ili kufanikisha zoezi.
Dkt
Warioba ameongeza kuwa shughuli hizo za sensa hazitaathiri shughuli zao
za kiuchumi na kijamii isipokuwa makarani wa sensa zitawachukua siku
zisizo zidi saba katika kutekeleza zoezi hili kuanzia tarehe 26 mpaka
tarehe 2.
Kwa
upande wao makarani hao wamesema wanashukuru kwa mafunzo waliyopatiwa
na wameahidi kuekeleza jukumu la sensa lililopo mbele yao kwani
wanatambua dhamana waliyokabidhiwa hivyo wamemuahidi mkuu wa wilaya kuwa
watafanikisha zoezi hilo kama inavyotegemewa na serikali na kutoa wito
kwa wananchi kujitokeza ili kuweza kufanikisha zoezi hilo.
Chanzo:Mzee wa Matukio Daima
Post a Comment