Baada ya Chama cha Mapinduzi kupigwa mwereka kwenye hukumu iliyosomwa na kutengeua matokeo ya Ubunge wa Igunga,tayari wameshaanza kunyoosheana vidole kwa kutafuta mchawi ni nani.Tayari makundi hayo yameanza kushutumu Rais Mstaafu Mkapa kuwa yeye ndie aliyechangia chama hicho kupigwa mwereka huko Igunga.Hivyo wameomba chama hicho kijitizame upya kinapoteua watu kushiriki kwenye kampeni.
Hukumu hiyo kwa upande wa CHADEMA imepokelewa kwa furaha kubwa huku kukijinasibu kuwa kitashinda kwa idadi kubwa ya kura iwapo uchaguzi huo utarudiwa siku yeyote ile.
Akihutubia maelfu ya wana igunga jana Katibu mkuu wa CHADEMA Dr.Slaa ambae amekuwa kwenye Operesheni Sangara huko mkoani Morogoro lakini jana akiwa Igunga alikituhumu chama tawala kuwa kitaumbuka iwapo kitakata rufaa kupinga hukumu hiyo.
Tayari CCM kilishatangaza kusudio lake la kukata rufaa hukumu hiyo wakisema chama hicho hakija tendewa haki.
Kushikana huku mashati ndani ya Chama Cha Mapinduzi huku kikiwa kwenye uchaguzi katika jumuiya zake ni dalili zilezile za makundi katika chama hicho yanavyozidi kutafunana huku makundi hayo yakijitafutia uhalali wa kushika nyadhifa mbalimbali katika chama hicho kuelekea uchaguzi Mkuu wa Chama na wengi wakiwa wanahitaji watu wao washike nyadhifa kuelekea pia Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Je haya tuyaonayo kipindi hiki tuyatarajie makubwa zaidi kadiri muda unavyokaribia mwaka 2015 ?
Loading...
Chediel . Powered by Blogger.
Post a Comment