TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA MAJI
TAARIFA KWA UMMA
Tarehe
9 Agosti 2012 Gazeti la Rai Na.995 katika ukurasa wake wa kwanza
lilichapisha taarifa yenye kichwa cha habari “Ufisadi Wizara ya Maji” na
kuwa Viongozi Waandamizi wanatumia mali za Serikali na taaluma zao kwa
maslahi binafsi. Gazeti hilo lilieleza kuwa walinzi wanashirikiana na
wafanyakazi kula “dili” za nje, habari hizi hazina ukweli wowote na ni
za kupotosha umma.
Maelezo
yaliyoandikwa katika uk.2 na 3 chini ya kichwa cha habari hiyo, hakuna
uhusiano wa Wizara ya Maji na ufisadi katika hifadhi ya eneo la
Ngorongoro ambayo inamhusisha Mh. Pius Msekwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM
kama Mwenyekiti wa Bodi hiyo. Kwa maoni yetu Gazeti la Rai linawajibika
kukiri kuwa kichwa cha Habari hiyo kilikosewa tena ukurasa wa mbele
(front page) kama ilivyoandikwa habari hiyo. Tunaheshimu Uhuru wa vyombo
vya Habari na tungependa kama kuna suala lolote linalohitaji ufafanuzi,
Wizara ipo tayari muda wowote kutoa maelezo badala ya kukimbilia
kuandika habari zinazojichanganya.
Imetolewa na:Katibu Mkuu WIZARA YA MAJI 10/8/2012
Post a Comment