JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Sued Kagasheki amebadili
taratibu za kuwapata wajumbe wa Bodi mbali mbali zilozoko chini ya
Wizara. Kuanzia sasa Wajumbe wa Bodi hizo watapatikana kwa njia ya
ushindani badala ya kuteuliwa moja kwa moja na Waziri.
Kwa sasa kuna Bodi nane (8) ambazo muda wake umeisha au unakaribia kuisha.Bodi hizo ni za za Taasisis/Mashirika yafuatayo;-
I. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
II. Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI)
III. Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI)
IV. Makumbusho ya Taifa
V. Chuo cha Mafunzo na Usimamizi wa Wanyamapori (MWEKA)
VI. Chuo cha Mafunzo ya Wanyamapori Pasiansi
VII. Wakala wa Mbegu za Miti (TTSA)
VIII. Bodi ya Leseni za Utalii (TTLB)
Watanzania wenye sifa za kuwa Wajumbe wa Bodi hizo wanatakiwa kupeleka maombi kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.
Maelezo zaidi ya namna ya kupeka maombi yataweka kwenye magazeti na tovuti ya Wizara, www.mnrt.go.tz
NB: BOFYA HAPA KAMA UNAHITAJI KUOMBA NAFAZI ZA UJUMBE WA BODI http://www.mnrt.go.tz
Post a Comment