Harufu ya kikwapa imekua tatizo kubwa kwa jamii yetu na
watu wengi wameizoea hiyo harufu kiasi kwamba hawajitambui kua wanatoa harufu. Watu
wengi wa nchi za nje wakija Tanzania wanalalamika kua harufu ya kikwapa
inawasumbua.
Harufu ya kikwapa inatokana na
sababu nyingi kama usafi wa mwili, chakula kama (Red meat). Mtu anapotoa jasho,
bacteria wanatumia nafasi hiyo kwenda kwenye jasho kujipatia chakula. Kadri
bacteria wanavyokua wengi, harufu nayo inazidi. Kuoga kunasababisha bacteria
kuondoka hasa kama unatumia sabuni inayoua hao bacteria (antiseptic soap).
Bacteria wanaokaa kwenye kikwapa wanazidi pia kama unatumia kitaulo cha kuogea
na kutokukifua vizuri na kuacha kisikauke. Hivyo unashauriwa kukianika nje
kikauke baada ya kuoga, pamoja na taulo ya kujifutia ili viondokane na bacteria
au kama inawezekana kufua kila siku.
Kwa sababu mtu hawezi kushinda
anaoga siku nzima ni bora kutumia njia za kukinga harufu ya kikwapa. Njia hizo
ni kama zifuatazo:
1.
Kutumia
deodorants au antiperspirants.
Deodorants zinasaidia kuondoa bacteria ambao wako kwenye kikwapa. Mara nyingi
hua zina harufu nzuri na kuna ambazo hazina. Kazi yake ni kufanya bacteria
wasikae kwenye kikwapa. Antiperspirants zinazuia jasho lisitoke kwa wingi.
Unapoenda kununua deodorant angalia yenye ingredient inayoitwa Aluminium chlorohydrate.
2.
Kutumia baking powder. Hii ni njia rahisi zaidi ambayo
inatumia gharama ndogo zaidi. Kuna
packet ya baking powder ambayo inauzwa bei chini ya shilling mia na itadumu kwa
muda hata wa miezi mitatu. Weka kidogo kwenye kiganja, changanya na maji halafu paka kwenye kikwapa baada ya kuoga.
Hii itazuia harufu ya kikwapa siku nzima.
3.
Vaa
nguo za kitambaa cha cotton au wool. Nina maana kwamba nguo ambazo ni synthetic
kappa polyester au nylon zinafanya mtu atoe jasho zaidi.
4.
Nyoa
nywele za kikwapa. Nywele zikiwa nyingi zinakua kama mtego wa bacteria na
kusababisha harufu.
5.
Kunywa
maji mengi. Maji yanasaidia kutoa sumu kwenye mwili na kusababisha harufu
kupungua.
6.
Oga
angalau mara mbili kwa siku na kusugua vizuri sehemu ya kikwapa.
7.
Vaa
nguo safi kila siku.
8.
Hakikisha
huna harufu ya kikwapa kabla ya kutumia perfume kali. Mchanganyiko wa harufu ya
kikwapa na perfume inatoa harufu mbaya zaidi.
Ahsanteni sana
Mdau Raheli
Via Issa Michuzi
Post a Comment