Tumia fursa hii kupigia kura vivutio vya Tanzania ili viweze kuwa
miongoni mwa maajabu saba ya asili ya bara la Afrika. Vivutio vya Tanzania
vinavyoshindanishwa na vingine tisa (9) barani Afrika ni Mlima Kilimanjaro, Bonde
la Ngorongoro,
na hifadhi ya Serengeti.
.................................
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imeutangaza Mlima Kilimanjaro, Bonde la
Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti kuwa ni vivutio vitakavyoshindanishwa
ili kupata maajabu saba ya asili ya Bara la Afrika.Mkurugenzi Mtendaji
wa TTB, Dk Aloyce Nzuki alisema jana jijini Dar es Salaam kwamba
mashindano hayo yatavishirikisha vivutio vya asili 12 kutoka Bara la
Afrika.Alisema Tanzania ndiyo nchi pekee yenye vivutio vingi vya utalii
na kwamba imepata nafasi ya kuvishindanisha vivutio vyake vitatu
Alisema hayo vivutio vya Tanzania kupaishwa Afrika ni jukumu letu Watanzania kufanya hivyo.
Pia unaweza kupata habari mbalimbali kuhusu utajiri wa maliasili nchini kwa kutemblea tovuti ya nchi inayoelezea pia vivutio vilivyopo nchini.Vilivyojaa kila kona na nchi ikikabiliwa na shinikizo la Wananchi kuvitangaza vivutio hivyo ili viweze kuiletea nchi mapato ya kutosha.
Tembelea pia tovuti ya mkoa wa Lindi ambayo nayo wameonysha vivutio vilivyopo huko katika sekata hii inayokabiliwa na changamoto nyingi.
Post a Comment