Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

DIWANI WA CHADEMA ATOA TAARIFA ZA UONGO.


Na Samson Chacha,  Tarime.


Diwani wa Kata ya Turwa tarafa ya Inchage kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Charles Ndessi Mbusiro amelalamikiwa na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime akiwemo Mwenyekliti Amos Sagara , Mkurugenzi Mtendaji Fidelis Lumato,, Mhandisi wa Wilaya Kasim Shaban  na Mkurugenzi wa Kampuni ya Gimunta Champion Traders bw, John Gimunta  kwa kutoa taarifa za Uongo za Kata Nyingine kwa Kudai kuwa Kampuni hiyo imelipwa zaidi ya  tsh Milioni 30 za Ujenzi wa Barabara mpya inayounganisha Vitongoji vya  Msati na Romori Km 1.5 kila Upande ambayo ipo Kata ya Sabasaba Wakati Kampuni hiyo haijalipwa Fedha hizo anazodai Diwani Ndessi ,

Wakitoa Ufafanuzi Ofisini kwake hapo Septemba 10 mwaka huu  Kuhusiana na Taarifa Walizodai za Uongo Zilizoandikwa na baadhi ya Vyombo vya habari  Jumatatu Wiki hii likiwemo  ( gazeti la Dira ) Viongozi hao wa Halmashauri Mwenyekiti Sagara na Mkurugenzi Mtendaji bw, Lumato na Mhandisi   Kasim  walisema kuwa " tumesikitishwa na taarifa zilizotolewa kwa Vyombo vya habari na Diwani wa Kata ya Turwa bw, Ndessi ya Kata nyingine ya Sabasaba, kuwa Halmashauri tumisha Mlipa Mkandarasai Gimunta Champion Traders  tsh Milioni kati ya 30,000,000/=  na Milini 50 ,000,000,/= za Ujenzi wa Barabara Mpya yenye Umbali wa KM 3 Kwa pande mbili zinazounganisha Vitongoji vya Msati na Romori na Kwamba Barabara  hiyo imejengwa Chini ya Kiwango huku akijua kuwa taarifa alizotoa ni za Uongo ",

Viongozi hao Walisema kuwa " Kampuni ya Gimunta Champion Traders ilipewa Tenda ya Kulima Barabara Mpya iliyokuwa ikitumika kupita Mifugo kwenda Shambani na kutumika Kuvuka kwenda Kitongoji cha Pili kati ya Msati na Romori , Kikao cha Halmashauri kilipitisha Kujengwa Barabara hiyo yenye Urefu wa Km , 3 , Kampuni ya Gimunta ilipata Uzabuni ya kujenga barabara hiyo tangu Mwezi March Mwaka huu 2012  , Mkandarasi huyo alianza Kazi ya Kusafisha Eneo ambapo amefyeka kwa gharama ya tsh 960,000/= Kungoa Visiki na Miti 83 iliyokuwa katikati ya barabara hiyo  Kukwangua Barabara  tsh 1,680,000/=  tshi 3, 320,000/= kungoa Mawe tsh 2,840,000/= ambapo Jumla ni tsh 8,800,000/= ambazo Fedha hizo zimelipwa Mkandarasi na Kuwalipa Vibarua waliokuwa Wakifanya Kazi ya awali ya kuandaa eneo la barabara hiyo , hatujatoa Fedha zaidi ya hiyo anayodai  Diwani Ndessi kuwa tumlipa fedha zote zaidi ya  tsh Milioni 5o na barabara haijalimwa Rasmi ",Walisema Viongozi hao wa Halamashauri hiyo,

Mkurugenzi wa Halamshauri hiyo bw, Lumato alisema kuwa " tulifanya Mkataba na Kampuni ya Gimunta Champion Traders  wenye Kumb, Namba LGA / 67/2011/2012/W/10/LOT/ 2  ya kulima barabara Mpya Km 3 Msati hadi Romori  kwa gharama ya tsh Milioni 55,544,000/=  Kuunda barabara tsh Milioni 6,000,000/= Kuweka Changarawe tsh Milioni 32,000,000/= na kujenga Karavati Moja  na tumeisha Lipa tsh Milini 8,880,000/= na Mkandarasi anatarajia kukabidhi Kazi yake Mwezi Oktoba mwaka huu mbali na kudai kuwa Mvua  zinazonyesha Wilayani hapa zinachngia kukwamisha Juhudi za Kulima barabara hiyo na Kama Mkandarasi akikwama kukamilisha Kazi yake kwa Mda uliowekwa inabidi akatwe Asilimia 0.12 kila Siku ya Mkataba aliyokwama kufanya kazi na baadaye huwa Mkataba unavunjwa kwa Mkandarasi yeyote anayekwama kukamilisha Kazi yake kwa Mda uliopangwa bila sababu Maalum " alisema Mkurugenzi huyo bw, Lumato ,


Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo bw Sagara alisema kuwa " hawa Madiwani Wenzangu Wanaingiza Mambo ya Siasa za Majukwaani na kuziingiza katika Utendaji na kutaka kuvuruga Kata zingine kwa Kuzusha taarifa za Uongo kwa nia ya kujitafutia Umaarufu ambao hauna Kichwa wala Miguu na kuwachonganisha Wananchi , Makampuni Wazabuni na Halmashauri yenyewe Kwa Mambo ya Uzushi na Uongo na kwa nia ya kutaka kukwamisha Juhudi za Maendeleo katika Halmashauri hiyo ,

Diwani wa Kata ya Sabasaba kupitia Chadema Christopher Chomete naye ameungana na Mwenyekiti wa Halamashauri Sagara na Mkurugenzi  kulaumu Diwani mwenzake bw, Ndessi kutoa taarifa za Uongo kuhusu Kata yake bila ya kuwa na Uhakika hali ambayo inaleta Uchochezi kati ya Watendaji wa Halamsahauri  , Madiwani na Wananchi kuwa Fedha zinazoletwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo zimeliwa huku bado hazichaliwa na Mradi bado ndipo unaanza ,

Diwani Ndesii alipotafutwa na Waandishi wa habari kutaka kuzungumzia kuhusu  Habari alizotoa  kuwa Halmashauri ililipa Kampuni ya Gimunta Champion Traders zaidi ya Milini 50,000,000/= na kulima barabara Chini ya Kiwango katika Kata ya Sabasaba , Diwani huyo hakuweza kupatikana kwani Simu yake iliita bila Majibu ,

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Gimunta Champion Traders bw. John Gimnta alisema kuwa " Nimesikitishwa na Hbari zilizoandikwa katika Vyombo vya Habari kuwa Kampuni yangu imelima barabara Chini ya Kiwango  na kulipwa Fedha na Halmashauri zaidi ya tsh Milioni 50 ,000,000/= ambapo Barabara yenyewe nimemaliza kungoa Visiki na Kukwangua Sijallima kutokana na Mvua zinazonyesha fedha tulizopokea ni tsh Milioni 8,880,000/= ambazo zimelipwa Vibarua waliongoa Mawe , Visiki , Kufyeka , Miti 83 mali ya Watu  pamoja na Kukwangua ," alisema Gimunta .


Mwisho,0788312145  ,0762219255
Chanzo:CCM Blog
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top