Maandamano nje ya Ubalozi wa Marekani nchini Misri
Kumezuka ghasia zaidi nje ya ubalozi wa Marekani mjini Cairo kati ya polisi na waandamanaji wanaokashifu filamu ambayo wanasema kuwa inakejeli imani ya Kiislamu.
Runinga ya Misri ilionyesha gari likiteketezwa moto na watu wengine wakikimbia vitoza machozi.
Balozi wa Marekani nchini Libya , Christopher Stevens, aliuawa .Wakati huohuo maafisa wa Marekani wanasema serikali ya nchi hiyo inachunguza ikiwa mashambulio ya jumanne kwenye ubalozi wa Marekani katika mji wa Libya wa Benghazi yalikuwa ni ya kupangwa au la .
Maafisa wa Marekani wameelezea mashambulio hayo kama yenye utata na yenye kupangwa kitaalamu na kuna tetesi kwamba makundi ya jihad huenda yalihusika .
Awali ilifikiriwa kuwa mashambulio hayo yalikuwa na uhusiano na maandamano ya kupinga filamu iliyokuwa inamkejeli Mtume Mohammed.
Takriban waandamanaji mia mbili wamekusanyika karibu na ubalozi wa Marekani mjini Cairo Misri kwa usiku wa pili kuelezea hasira yao juu ya filamu hiyo .
Aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Libya Christopher Stevens
Awali waandamanaji walirusha mawe kwenye ubalozi huo na vikosi vya usalama vikafyatua mabomu ya kutoa machozi kuwa tawanya.
Watu wenye silaha waliokuwa na maguruneti walichomo moto jengo la ubalozi na walioshuhudia wanasema watu hao walizingira eneo hilo.
Rais Obama amelaani vikali shambulio hilo na ameahidi kushirikiana na serikali ya Libya kuwafikisha mbele ya sheria wahusika

This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
Jamii
on Thursday, September 13, 2012
Post a Comment