Chama Cha Wananchi(CUF) kimezindua Mchakamkacha wa Dira ya Mabadiliko(V4C) ili kuweza kuwafikia Wanachama wake popote pale walipo nchini na kuweza kuwavutia wengine wapya katika harakati zake za kujijenga upya.
Mkutano huo uliohutubiwa na Mwenyekiti wa Taifa Prof.Lipumba ulijaa kila aina ya shamrashamra uwanjani hapo Jangwani.
Lakini jambo kubwa lililoniacha hoi ni pale katika mchakamchaka wa kuchangisha fedha ambapo walipata takribani Sh 129 Milioni Mwenyekiti Pfor.Lipumba alisema maneno ambayo wakati yana ukakasi katika azma nzima ya vyma kuiondoa madarakani CCM alisema''
“Tunakwenda kuvunja ngome ya Chadema inayosifiwa, Arusha ni jiji linalohitaji utulivu wa kisiasa kwa kuwa ni kivutio cha wawekezaji" - Profesa Lipumba,
Sote tunajua kuwa vyama vya upinzani dhamira yao kubwa au adui yao mkubwa kisiasa ni chama kile kilicho madarakani na kwa hapa kwetu ni Chama Cha Mapinduzi(CCM),Lakini kauli hiyo ya Mwenyekiti inatufanya turejee nyuma kidogo Pale tulipokuwa tunasikia maneno kama ''CCM B'' nk.Pia yamekuja kipindi ambacho ni tarehe 20/9/2012 rufaa ya kupinga hukumu ya kutengua Ubunge wa Bwana Lema itakaposikilizwa.
Hivyo basi wengine tunatatizwa na maana halisi ya maneno hayo ya Mwenyekiti huku tukijua kabisa CUF na CHADEMA ni vyama vinavyotakiwa kuunganisha nguvu japo vinasita ili viweze kukabiliana na CCM vizuri na kupata matokeo mazuri katika chaguzi mbalimbali hapa nchini.
Lakini badala ya kuangalia namna ya kuunganisha nguvu CUF na CHADEMA wao wamekuja na wazo tunaloweza kusema hapa wamekengeuka wameamua kupambana na adui ambae kiuhalisia sio adui yao.
Pia inakuwaje wamekuja kipindi hiki rufaa ya Bwana Lema ikiwa karibuni kusikilizwa/kusomwa ?
Kwanini pia msisitizo utiliwe tu Arusha pana nini pale ?
Chama Cha Wananchi ni chama kilichowahi ng'ara katika medani za kisiasa hapa Tanzania Bara na kikajikuta kinapoteza umaarufu wake huo uliokuwepo kisa hasa Viongozi wao wanalo la kutuambia nini hasa kiliwakuta CUF hapa Bara.
Mkakati wao ni sawia kabisa kwani kila chama kinatakiwa kijiimarishe kwa kuwa na wanachama wa kutosha na hilo nawapongeza LAKINI shida yangu kuu imekuwa huu mkakati wao wa kuamua kukibomoa CHADEMA huko Arusha na inawezekana si Arusha tu watapita kila kona wakipambana na CHADEMA kama Mwenyekiti alivyosema huku wakimsahau adui yao wa kisiasa CCM wanaye takiwa kupambana nae,hii inatoa tafsiri nyingine kabisa na maswali ni mengi,,,,
Sisi tulio nje tunaona CUF inabidi makakti wao huu uangaliwe upya ifanye kazi ya kusaka wanachama na kujiimarisha sio kubomoana ninyi kwa ninyi.
Mchakamchaka huu wa CUF ni kwa ajili ya nani haswa ?
Nashukuru sana Mkuu wa Rundugai kwa kunipa nafasi kuelezea dukuduku langu hilo
Mdau wako
Rams Beka
ramsbeka@gmail.com
Post a Comment