Mkutano wa viongozi wa vilabu vya ligi kuu ya Tanzania bara uliofanyika jana jioni umemalizika na kutoa maamuzi ya pamoja kwamba vilabu hivyo hivyo vinavyoshiriki ligi kuu ya msimu huu haviutambui mkataba wa udhamini wa ligi uliosaniwa na Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini Bwana Angetile Osiah.
Katika mkutano huo ambao uliudhuriwa na takribani viongozi waote wakuu wa vilabu, umeamua kuchukua maamuzi ya kutoutambua mkataba huo na pia wameamua kwamba ndani ya siku 7 zijazo watakutana na kampuni ya simu ya Vodacom kwa ajili ya kujadili upya mkataba wa udhamini wa ligi kuu.
Vilabu pia kwa kauli ya pamoja wameagiza kwamba Katibu mkuu wa TFF, Angetile Osiah awaandikie barua kampuni ya ya Zantel ambao ndio wadhamini wa klabu ya African Lyon kwamba mkataba wao wa udhamini usimamishwe kwa kipindi cha siku saba ili kuweza kuweka mambo sawa .
Kwa maana siku saba zijazo kuanzia Jumatano ya leo, umoja wa vilabu hivyo vitatoa tamko rasmi juu ya masuala yote ya udhamini wa ligi kuu na namna jinsi suala la udhamini wa Zantel kwa African Lyon utakavyokuwa.
Pia katika hatua nyingine kumekuwepo na taarifa kwamba Mwenyekti wa kamati ya mchakato wa kuunda kampuni ya ligi kuu, makamu Mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange Kaburu ataondolewa katika nafasi hiyo kutokana na tuhuma za kutokuwa na umoja na viongozi wenzie wa vilabu katika kupigania maslahi ya vilabu vyote.
Mtu anayepewa nafasi ya kuchukua nafasi ya Kaburu ni makamu mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga.
Chanzo:Shaffih Dauda
Chanzo:Shaffih Dauda
Post a Comment