Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WAKATI SIMBA NA YANGA WAKIHANGAIKA NA TWITE NA YONDANI BONGO,MAN CITY WAJA NA MPANGO WA KULITAWALA SOKA LA ULAYA

 Manchester City Miaka miwili ijayo watakuwa wamekamilisha mpango wao huu ambao nia yao kubwa ni kuja kuwa Klabu inayotisha zaidi katika Soka la Ulaya na mradi huu wa viwanja vya Mazoezi kwa rika zote kuanzia vijana wadogo unatarajiwa kukamilika mwaka 2014

 Usiku na Mchana viwanja hivyo vitatumika ni katika jumla ya viwanja 17 ambapo viwanja 12 vitatumiwa kwa ajili ya timu za Vijana ambapo timu hiyo imedhamiria kuondokana na usajili wa bei mbaya na kukuza vipaji vyao wenyewe ili kuweza kuwa na staili moja ya uchezaji katika mpango wao wa kulitawala soka la Ulaya na kuwa Klabu kubwa katika Ulimwengu wa Soka 

 Katika eneo hilo la eka 80 klabu hiyo imetenga eka 6 kwa ajili ya shughuli za kijamii .
Mipango hiyo ni kutokana na uongozi wa Klabu hiyo kuona umuhimu wa kupika vipaji vyao wenyewe kuliko kuingia katika sokola usajili ambalo huwa ghali sana kwa wale wachezaji wenye vipaji hivyo kuondokana na hali hiyo Man City wameamua sasa Kujenga eneo litakaloigharimu Klabu hiyo Paundi 80M litakuwa na viwanja vya kuchezea 17,kiwanja chenye uwezo wa kuingiza watu 7,000 kwa ajili ya mechi za timu ya akiba.

Hapa Bongo ukiangalia mipango ya Klabu zetu kubwa ambazo ni za kuonyeshewa mfano zenyewe zimekuwa bingwa wa kuonekana kwenye vyombo vya habari zikipambwa kwa mbwembwe  kuwa yule kasajili bonge la beki huyu kapata fowadi la kufa mtu ilimradi vurugu mechi.

Timu hizi zinaingia viwanjani hususani mechi za kaimataifa hatuoni huo ubunge wa beki na huyo fowadi wa kufa mtu kama wana la ziada wamebaki kuwa timu za magazetini.Zimekuwa zikifanya vibaya nje na ndani ya uwanja.

Wamekuwa wapiga porojo kila siku na timu zao kuwa katika hali mbaya kila sekta tumeona baadhi ya mifano wa Kujenga uwanja mpya ambao ulipigiwa chapuo lakin mpaka sasa kimyaa sijui umeishia wapi. Hata watani wao pia waliwahi kuja na porojo za namna hii pale nao waliposema watajenga uwanja mpya pale pale walipo na uwanja wao wa sasa hii imekuwa kawaida ya soka letu.

Man City wameonyesha jinsi Klabu hiyo  ilivyo na kiu ya Kweli ya Mataji Wakati Simba na Yanga wakibakia na porojo zile zile kila mwaka.

Tuwapongeze Azam Fc kwa jitihada zao kubwa wanazozifanya na kuonekana kuwa ni Klabu ya dhamira ya dhati ya mafanikio.



author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top