Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

SIMBA 2-2 KAGERA SUGAR


 DK:90 SIMBA 2-2 KAGERA
  DK 80:wachezaji wa timu zote wanajaribu kupenya ngome ya mwenzake japo wanakosa maarifa ya kuweza kupata bao huku dakika zikiyoyoma
 Kagera Sugar wanapata uhai hapa baada ya kuweza kusawazisha magoli mawili huku Simba nao wakitafuta goli la ushindi.

 DK 75: Wanasawazisha SIMBA 2-2 KAGERA SUGAR
           Kagera wanapata penati baada ya mabeki wa Simba kumuangusha mchezaji wa kagera ndani ya    18Salum Kanoni ndie anapiga
DK:65 Kagera Sugar wanapata bao Felix Semi

DK 57: Emmanuel Okwi anaingia vizuri kutokea pembeni na kuwatoka mabeki wa Kagera anapiga shuti kali na kipa anaokoa kwa ustadi mkubwa.

DK 50 Mrisho Ngassa anaifungia Simba bao la pili baada ya kupata pande maridadi kutoka kwa Okwi

DK 45: Kagera Sugar wanaonekana kuwaelemea Simba ndani ya dakika za mwisho za kipindi cha kwanza, wanafanya shambulizi kali lakini Juma Kaseja anaifanya kazi yake vizuri ya kulinda lango la mnyama.

 DK 44: Simba 1 - 0 Kagera Sugar

 DK 37: Simba 1 - 0 Kagera Sugar

 DK 32: Haruna Moshi Boban anakosa bao la wazi baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Okwi.

DK 30: Timu zote zinashindana kumiliki mpira ingawa Kagera wanaonekana kuwazidi Simba kiasi, lakini Kagera wanakosa mipango mziru ya kuweza kupitisha mipira mbele ya Kaseja na kusawazisha goli.

 DK 22: Chollo anapiga krosi safi inayomfikia Sunzu anayepiga kichwa lakini anashindwa kulenga goli na mpira unatoka nje.

DK 20: Simba 1 - 0 Kagera Sugar

DK 13: Mpira sasa uanaanza kubadilika baada ya Simba kupata goli, Kagera nao wameamka na kuanza kujibu mashambulizi.

DK 8: Felix Sunzu anafunga bao safi la kichwa hapa uwanja wa taifa baada ya kupata krosi maridadi kutoka kwa Ngassa. Simba 1 - 0 Kagera Sugar.

 DK 5: Mchezo umeanza kwa kasi na Simba wanaonekana kulishambulia zaidi lango la Kagera wakifika mara kadhaa ndani ya sita ya Kagera lakini bado hawajatengeneza nafasi nzuri ya kufunga.


WALIOANZA SIMBA NI:
Kaseja, Chollo, Maftah, Nyoso, Ochieng, Kazimoto, Ngassa, Kiemba, Sunzu, Boban, Okwi.

Walianzia benchi;
Mweta, Ngalema, Hassan Hatibu, Jonas Mkude, Uhuru, Kinje na Edward Christopher
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top