Klabu ya Liverpool ya Uingereza imekanusha vikali taarifa ya mchezaji wa zamani wa Juventus mkongwe Del Piero aliyenukuliwa na gazeti moja nchini Italia kuwa alikataa kujiunga na vijogoo hao wa Arnfield kutokana na kuogopa kuwaudhi mashabiki wa Juventus kutokana na kufariki dunia kwa mashabiki wao 39 mwaka 1985.
Liverpool wamesema hawakuwa na nia nae kutokana na umri wake hivyo hakuwa katika mipango ya Kocha Brendan Rodgers.Hivyo hakuna afisa yeyote aliyewahi kuongea na Alessandro Del Piero wala wakala wake na habari hizo ni za uongo.
Hivyo Klabu hiyo imesema wale waliongea nae walikuwa na nia tu ya kutengeneza vichwa vya habari katika magazeti yao,kutokana na sera ya Klabu hatukuwa katika maongezi kufikia hatua ya kutua katika klabu.
Phil Neal (kushoto), Michel Platini na Ian Rush (Kulia) wakiwa na ngao katika juhudi za mahusiano mema 2005 kabla ya mpambano wao.
Klabu hiyo imesema imekuwa ikifanya kazi na Juventus katika kurudisha uhusiano mwema kati ya timu hizo mbili kutokana na tukio la Heysel la mwaka 1985 ambapo mashabiki 39 wa Juventus walifariki dunia katika mechi kati ya Juventus na Liverpol.
Post a Comment