Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MFUMUKO WA BEI WAFIKIA ASILIMIA 13.5



OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema mfumuko wa bei za bidhaa nchini, umepungua kutoka asilimia 14.9 Agosti hadi asilimia 13.5 Septemba Mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma  iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mkuu NBS, Dk Albina Chuwa, mfumuko wa bei ulianza kushuka kutoka asilimia 19.7  Januari hadi asilimia 13.5  Septemba, mwaka huu.

Dk Chuwa alisema kupungua kwa mfumuko wa bei mwezi uliopita kunamaanisha kuwa, kasi ya upandaji bei za bidhaa na huduma kwa mwezi huo uliendelea kupungua.

“Mfumuko wa bei wa vyakula na vinywaji baridi umepungua hadi kufikia asilimia 15.6  Septemba kutoka asilimia 18.8  Agosti mwaka huu” alisema Dk Chuwa.

Aliongeza bei za bidhaa za vyakula majumbani na mighawa imepungua hadi asilimia 15.8  Septemba ikilinganishwa na asilimia 18.5 Agosti.

Dk Chuwa alisema bei kwa bidhaa zisizo za vyakula imeongezeka kidogo hadi asilimia 10.5 mwezi uliopita, ikilinganishwa na asilimia 10.3  Agosti mwaka huu.

“Mfumuko wa bei ambao haujumuishi vyakula na nishati kwa mwezi uliopita,  umepungua hadi asilimia 8.9 ikilinganishwa na asilimia 9.2 Agosti mwaka huu,” alisema Dk Chuwa.

Aliongeza kuwa mfumuko wa bei ya nishati kwa mwezi uliopita, umeongezeka hadi kufikia asilimia 19.4 ikilinganishwa na asilimia 16.9 Agosti mwaka huu.

Alisema kuongezeka kwa mfumuko wa nishati kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei za petroli kwa asilimia 11.4 na dizeli kwa asilimia 6.8 Agosti hadi mwezi uliopita.

Dk Chuwa alisema mfumuko wa bei kwa nchi jirani kama Kenya, umekuwa ukishuka kutoka asilimia 6.09 Agosti  mwaka huu hadi asilimia 5.32 mwezi uliopita.

Uganda mufumko ulifikia asilimia 5.4 mwezi uliopita kutoka asilimia 11.9 Agosti mwaka huu na Zambia umetoka asilima 6.4 Agosti na kufikia asilimia 6.6 mwezi uliopita.
Chanzo:www.mwananchi.co.tz
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top