Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu
,,,,,,,
Kwa ufupi
Alisema hadi sasa kuna mawakala wanaotoa huduma za
fedha kwa njia ya simu za mikononi wapatao 138,000 nchi nzima na kadi za
simu zilizosajiliwa zipatazo milioni 20 na hivyo kufanya huduma
kufanyika katika mazingira yanayojitosheleza.
Akizungumza na waandishi wa habari jana
mjini Arusha baada ya kutoa utangulizi wa mkutano wa taasisi za fedha,
Profesa Ndulu alisema teknolojia ya kutumia simu katika kutuma na
kupokea fedha, imekuwa kwa kasi na inapatikana katika maeneo mengi
yakiwemo ya vijijini ambako huduma za benki si za kuridhisha.
Alisema mpango wa benki kutoa huduma kwa njia ya simu za mkononi, utaokoa gharama kwa benki nyingi kwani gharama za sasa za kufungua tawi moja ni si chini ya Sh400 milioni.
“Huduma hii ni nzuri sana kwa watumiaji kwa sababu ni salama,gharama zake ni za chini na zinaongeza ushindani hivyo kufanya mtumiaji kupata huduma kwa gharama nafuu,”alisema Profesa Ndulu.
Alisema hadi sasa kuna mawakala wanaotoa huduma za fedha kwa njia ya simu za mikononi wapatao 138,000 nchi nzima na kadi za simu zilizosajiliwa zipatazo milioni 20 na hivyo kufanya huduma kufanyika katika mazingira yanayojitosheleza.
Alisema utaratibu huo utaziwezesha benki kwa kushirikiana na mawakala walisambaa maeneo mbalimbali nchini, kuwafungulia wateja wao akaunti za benki na kupata huduma ya kuweka na kutoa fedha bila ya kuwepo kwa tawi la benki husika.
Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kufunguliwa na Rais Jakaya Kikwete na utahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa taasisi za fedha kutoka maeneo mbalimbali nchini
Chanzo:Mwananchi.
Post a Comment