Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akisalimiana na
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Balozi Peter Kallaghe, wakati
alipowasili katika hafla ya chakula cha jioni katika yake, Balozi na
maaofisa wa Bodi ya Utalii na Taasisi zake pamoja na maofisa wa ubalozi
wa Tanzania nchini Uingereza ili kuagana na kutathimini mapungufu na
mafanikio ya ushiriki wa Tanzania katika maonyesho ya dunia ya utalii
World Treavel Market (WTM) yaliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita
nchini Uingereza, ambapo zaidi ya makampuni 55 yanayouza na kutangaza
utalii wa Tanzania yalishiriki katika maonyesho hayo, maonyesho hayo
hufanyika kila mwaka eneo la Excel jijini London.
Balozi Khamis Kagasheki aliitaka Bodi ya Utalii Tanzania kuongeza juhudi
zaidi ili kuleta mafanikio zaidi katika maonyesho hayo na menine na
kuongeza idadi ya watalii kufiki milioni moja kwa mwaka, Tanzania
ikijipanga vizuri na kutangza vivutio vyake zaidi duniani inaweza kupata
mafanikio zaidi katika utalii na kuongeza zaidimapato yake ikiwa ni
pamoja na kukuza uchumi kupitia sekta ya utalii.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika
hafla hiyo ambapo aliwashukuru maofisa kutoka Bodi ya Utalii na Taasisi
zake pamoja na makampuni yaliyoshiriki katika maonyesho hayo kwa
maandalizi mazuri katika ushiriki huo, lakini pia akaagiza kuangalia
changamoto na kuzifanyia kazi ili kuboresha zaidi ushiriki wa Tanzania
katika maonyesho yajayo na mengine yanayoweza kufanyika katika nchi
zingine, kulia katika picha ni Balozi Peter Kallaghe na kulia ni Mama
Balozi
Picha na Fullshangwe Blog
Post a Comment